Monday, June 4, 2012

SAJENTI AKANA TUHUMA ZA CHARLES BABA

Mzazi mwenza wa Mwanamuziki Charles Baba, Husna Idd (Sajent) pichani, ameibuka na kukana tuhuma alizozitoa baba huyo wa mtoto wake wiki mbili zilizopita kuwa Sajent ana tabia ya kugombana na kila msichana anayeanzisha uhusiano na baba mtoto wake huyo. Akizungumza na Blog hii Sajent alisema kuwa amesikia madai hayo ya Charles Baba na kudai kuwa maneno hayo ni ya kizushi kwa kuwa yeye anatambua kuwa walishamwagana na Charles siku nyingi hivyo hawezi kugombana na mwanamke wa Charles kwa sasa kwa kuwa anamchukulia mwanaume huyo kama baba wa mtoto wake tu na si vinginevyo. Husna ameongeza kuwa Charles na wanawake wake huwa wanajishtukia kila wamuonapo kutokana na uzuri alionao nakukiri kuwa yeye ni mzuri hivyo huwapiga kwa kutumia uzuri alionao na si kwa ngumi.

No comments:

Post a Comment