Thursday, June 7, 2012

SIJAWAHI KUTEMBEA NA JACK PENTZEL WALA SHILOLE-TIMBULO

Timbulo
Msanii mchanga ndani ya Game la Bongo Flava na aliyepata kashfa kwa kucopy nyimbo za watu, Timbulo amekanusha uvumi uliopo kuwa ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na dada zake, Jack Pentzel maarufu Jack wa Chuz pamoja na mwanadada anayekimbiza kwenye Game la muziki Bongo na Filamu za kitanzania.. Kabla ya kuibuka na kukanusha uhusiano huo huko nyuma kulikuwa na uvumi wa Dogo huyo kutoka na Shilole na baadae kuhamia kwa Jack na kwa nyakati tofauti wadada hao walikiri kuwa na uhusiano na mdogo wao huyo ambapo Jack alithibitisha kuwa wanaishi pamoja na wanapika na kupakua lakini ghafla zikasikika habari kuwa wawili hao tayari wamemwagana.  Cha ajabu Timbulo aliwekwa kati jana na kipindi cha HOTMIX cha Eatv na kukana hayo yote kwa kusema ni maneno ya uzushi yanayolenga kumharibia kisanaa.. (Picha ya chini inamuonyesha Timbulo akiwa na Jack katika pozi la kimahaba)

No comments:

Post a Comment