Wednesday, June 20, 2012

HUU NI USHINDANI AU NI MAENDELEO TU

X6 inayotumiwa na Jack Wolper ambayo inadaiwa kuwa amenyang'anywa

Siku chache zilizopita Msanii wa filamu Bongo Jacqline Wolper aliutangazia Umma gari yake mpya anayoitumia aina ya X6 na tetesi nyingi tukazisikia huko mtaani na kwenye baadhi ya vyombo vya habari moja ya tetesi hizo ni kuwa gari hiyo si yake ila amepewa na mwanaume na lakini ghafla likaibuka jingine kuwa Wolper amenyang'anywa gari hiyo na huyo aliyempa


Kabla halijasahaulika hilo ghafla zikasikika habari katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa Wema Sepetu kwa sasa anamiliki gari nyingine aina ya Mark X badala ya ile Lexus hapo juu pamoja na nyumba anayoishi sasa ambayo pia ni mali yake.
 Wakati hayo yakiendelea jana kwenye Website yake mwana bongo Flava Diamond Da Platinumz ametupia gari yake mpya na kuwaambia mashabiki wake wanaoitembelea Website hiyo kuwa waishuhudie kisha wakawasimulie wenzao.. Sasa jamani huu ni ushindani au Maendeleo maana kila mmoja akinunua gari, nyumba anakimbilia kwenye vyombo vya habari hawa watu wako kwenye mashindano au wanajaribu kutuonyesha kuwa sanaa bongo inalipa au ni njia ya kutuhamasisha vijana wenzao tujitume ili tupate maendeleo kama ya kwao? Sijui!!!!!

No comments:

Post a Comment