Wednesday, June 20, 2012

KUTOKA UTANGAZAJI MPAKA UIGIZAJI NA KOTE ANAKAMUA

Mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na kituo cha EATV, Abdallah Hamis Ambua a.k.a Mjukuu amefunguka kuwa pamoja na kufanya vizuri kwenye Utangazaji lakini pia ana vipaji lukuki ambapo kwa sasa ameibukia kwenye uigizaji. Akizungumza na kipindi cha HOTMIX cha Eatv kinachoruka kila Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 11 jioni, Dullah amesema pamoja na utangazaji pia ana vipaji vingi kama vile uigizaji ambapo kwa kutambua hilo ameamua kujikita huko na tayari ameshafanya Filamu ya Jeraha la moyo ambayo tayari iko sokoni na Filamu ya Glory of Ramadhan iliyotayarishwa na kampuni ya RJ inayoongozwa na Vicent Kigosi(Ray) ambayo itatoka hivi karibuni. Dulla amewataka mashabiki wake wa Planet Bongo wampokee vizuri kwenye Soko la filamu na anaahidi kufanya makamuzi kwenye pande zote yaani utangazaji na uigizaji.
 
 

No comments:

Post a Comment