Tuesday, January 31, 2012

MASHAUZI CLASSIC YAACHIA SI BURE UNA MAPUNGUFU

Kundi la muziki wa Taarab linalotikisa anga ya muziki huo nchini Tanzania "Mashauzi Classic" limeachia wimbo mpya walioupa jina la "Si bure una mapungufu

Akizungumza na Eatv kupitia kipindi cha Afrobeat Mkurugenzi wa kundi hilo Isha Ramadhani a.k.a Isha Mashauzi amesema Katika wimbo huo, wamemzungumzia mtu mwenye majivuno anayejiona anajua kila kitu, asiyependa maendeleo ya wenzake, asiyependa kukosolewa na mwenye kupenda kutukuzwa siku zote lakini hastahili hayo yote.

Na haya ni baadhi ya mashairi yaliyomo kwenye wimbo huo “Tulivyokuzoea tofauti na ulivyo, tuna wasiwasi ni mwezi mchanga, mambo yako sera zako sasa hivi ni ovyo, mara karudi tena kwa waganga, si bure una mapungufu tunakuhurumia, umekuwa kama fukufuku kila shimo waingia” 

Aidha Isha amefafanua kuwa kama ilivyo kawaida ya nyimbo zake, kwenye mashairi ya wimbo huo hakumlenga mtu yeyote isipokuwa amesimama kama msanii ambae ni mwakilishi wa wale wote wanaokerwa na watu wenye tabia kama hizolakini hawana nafasi ya kuzifikisha kero zao hivyo litakayemgusa basi linamhusuuu.....

No comments:

Post a Comment