Sunday, January 29, 2012

AFROBEAT NDANI YA DAR LIVE-MBAGALAA

Hapo ni kabla ya kuanza kipindi, nikipata maelekezo kutoka kwa Producer wangu (Mussa Kondo) na huyo dogo hapo ni mtoto wangu Harison a.k.a Obama akifuatilia mama yake anavyopewa maelekezo
Kazi ikiendelea na kama unavyowaona hao watoto nao wakitaka waonekane kwenye kipindi na hii ni moja ya Changamoto kubwa sana ambayo tunakabiliana nayo tunapokuwa kwenye Location kama hizi zenye hadhara ya watu hasa watoto.
Hapo dogo nae aking'ang'ania Mic ikabidi tumpe kidogo ili tumridhishe nasi tuweze kuendelea na kazi, maana bila hivyo hapo anaangusha kilio mpaka kazi yenyewe unaiona chungu
Hapo sasa kazi imeanza na hii sehemu ndo niliitumia kwa kufungua na kufungia kipindi
Hapo kazi ikiendelea na kama unavyoona hapo juu ni mama akipiga mzigo na chini ni dogo Herry  nae katulia akimfuatilia mother wake kwa umakini mkubwa
Hii ndiyo Crew nzima ambayo imeweza kukamilisha Show hiyo ambayo utaiona Jumamosi hii huyo mwenye Bag ni Soundman anaitwa Jacob anaefuata ni Producer Mussa Kondo na anayeonekana kidogo ni Rajab kimanyo (Cameraman) wakiwajibika.





No comments:

Post a Comment