Monday, January 30, 2012

SIKU ZA WEEKEND HUWA NI KAZI TU KWA KWENDA MBELE


Kama nilivyoeleza hapo juu kuwa siku za Weekend zinakuwa ni siku za kazi zaidi kwa Team ya Afrobeat hivyo baada ya kutoka Dar Live tulielekea Temeke Davis Corner kwa ajili ya Interview na kiongozi wa Coast Modern Taarab Omary Tego(na hicho ndicho kiti alichokitumia Tego) kitu cha vidole vitano, Halla Five Nyalifa umeiona hiyoooo???
Hapo Omary Tego akijibu maswali niliyokuwa nikimuuliza
Mahojiano yakiendelea kikubwa hasa ambacho tulitaka kufahamu ni kuhusu Kundi lake maana inasemekana kuwa baada ya baadhi ya wanamuziki wake kuondoka, kundi hilo limeyumba sana na linaelekea kufa kabisa ambapo mwenyewe amekanusha madai hayo na kudai kuwa kundi lake bado liko fresh kwa sababu bado lina wanamuziki wengi tu ambao ni wakali na wanafanya kazi nzuri kama ilivyokuwa mwanzo
Crew ikiwajibika kama kawa Cameraman Rajab Kimanyo sambamba na Soundman Jacob
Baada ya mahojiano mazungumzo na story za hapa na pale ziliendelea, kushoto ni Producer wa Afrobeat, Mussa kondo na Omary Tego
Omary akijiachia na Mutoto muzuri
Tukaambiwa aah mbona mnaogopana jamani?? ikabidi tusogeleane kidogoo.. hhahahahahhaa ni picha tu jamani msije mkazusha mengine maana wale ndugu zetu tunawajua wenyewe.
My Producer nae akasema aah mbona mwajipendelea!!! akasogea na yeye tukajifotoaa.. Endelea kuangalia Afrobeat ili usipitwe na mambo haya mazuri jamani, only on Eatv the no. 1 Youth Channel

No comments:

Post a Comment