Wednesday, February 20, 2013

MTOTO WA MIAKA 6 AFARIKI DUNIA NCHINI UGANDA BAADA YA MAMA WA KAMBO KUFUNGIA WATOTO NDANI NA KUCHOMA MOTO NYUMBA

Baba wa watoto hao Kanakulya akiwa na mmoja wa watoto zake aliyeokolewa katika janga hilo.(Picha kwa hisani ya newvision.co.ug)


Mtoto asiye na hatia amefariki dunia baada ya mama yake wa kambo kumfungia ndani ya nyumba pamoja na ndugu zake watatu wakiwa wamelala kisha kuchoma nyumba hiyo moto.


Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku katika kijiji cha Namuyenje kilichopo katika wilaya ya Mukono.


Mtoto Shafik Jjuuko mwenye umri wa miaka 6 alifariki kwa kukosa hewa wakati mama yake wa kambo Margareth Nampiima mwenye umri wa miaka 27 alipochoma moto nyumba waliokuwemo watoto hao huku baba yao ambaye ni dereva akiwa safarini.

Watoto wengine Sulaiman Mutebi 8, Shamim Nakimera, 9 na Hassan Geserwa 11 waliokolewa wakiwa na majeraha yaliyosababishwa na moto huo ambao pia umeteketeza mali kadhaa.

source:
newvision.co.ug

No comments:

Post a Comment