Thursday, February 28, 2013

ZAWADI ZA MPINGA CUP ZATAJWA

Kiongozi mkuu  maandalizi ya Mashindano ya Mpinga Cup ametangaza zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa timu zitakazoshiriki katika michuano ya Mpinga Cup inayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama bodabado wa jijini dar esa saalam yanayotegemea kufanyika leo katika viwanja vya Oysterbay police kwa muda wa wiki moja.

Akitangaza zawadi hizo ASP Emilian Kamwanda ambaye ni msaidizi Mwandamizi wa polisi na Kiongozi wa maandalizi ya michuano ya mpinga cup alisema” leo tunayo furaha kutangaza zawadi mbalimbali za washindi katika mashindano hayo ambayo yana lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikiki (bodaboda). Na zawadi hizi ziko kama ifuatavyo.

Mshindi wa kwanza atapata Kombe, Pesa taslimu shilingi million moja, jezi  set moja, kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1, mshindi wa pili atapata pesa taslimu shilingi laki tano, jezi seti moja , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1 na mshindi wa tatu atapata  pesa taslimu shilingi laki tatu, , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1,Aidha zawadi zitatolewa kwa Mchezaji bora na Goalkeeper bora ambapo  kila mmoja atapata  pesa taslimu shilingi laki moja,  vocha za kufanya manunuzi Mr Price zenye thamani ya Laki moja na kofia ngumu (helmet) 1.Timu tano zitakazoshindwa pia hazitaondoka hivihivi , zitazawadiwa kila moja mipra na kofia ngumu Helmet.
Mashindano ya Mpinga Cup yameandaliwa na Jeshi la polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel, Rotary club, Mr.Price, Home Shopping Center  pamoja na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ili kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya sheria mbalimbali za usalama , kuimarisha uelewa wao wa matumizi ya barabara kwa lengo la kuendelea kudhibiti  ajali za barabarani pamoja na elimu ya Polisi jamii.

Mashindano haya yanatarajiwa kutimua mbio kuanzia tarehe leo katika viwanja vya Polisi Oysterbey   kwa kushirikisha timu 8 za waendesha pikipiki. Mpinga Cup itaendelea katika mikoa ya Kipolisi ya Ilala na Temeke na hatimaye kutafuta mshindi wa mkoa wa Dsm.

 SOURCE: 
http://mrokim.blogspot.com

Wednesday, February 20, 2013

MTOTO WA MIAKA 6 AFARIKI DUNIA NCHINI UGANDA BAADA YA MAMA WA KAMBO KUFUNGIA WATOTO NDANI NA KUCHOMA MOTO NYUMBA

Baba wa watoto hao Kanakulya akiwa na mmoja wa watoto zake aliyeokolewa katika janga hilo.(Picha kwa hisani ya newvision.co.ug)


Mtoto asiye na hatia amefariki dunia baada ya mama yake wa kambo kumfungia ndani ya nyumba pamoja na ndugu zake watatu wakiwa wamelala kisha kuchoma nyumba hiyo moto.


Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku katika kijiji cha Namuyenje kilichopo katika wilaya ya Mukono.


Mtoto Shafik Jjuuko mwenye umri wa miaka 6 alifariki kwa kukosa hewa wakati mama yake wa kambo Margareth Nampiima mwenye umri wa miaka 27 alipochoma moto nyumba waliokuwemo watoto hao huku baba yao ambaye ni dereva akiwa safarini.

Watoto wengine Sulaiman Mutebi 8, Shamim Nakimera, 9 na Hassan Geserwa 11 waliokolewa wakiwa na majeraha yaliyosababishwa na moto huo ambao pia umeteketeza mali kadhaa.

source:
newvision.co.ug

KAMA UMEGUSWA MCHANGIE MTOTO HUYU AWEZE KUTIBIWA

Mtoto Ombeni Mbeula akiwa hospitali kama umeguswa na hali ya mtoto huyu tafadhari tuma chochote kwa njia ya M-Pesa 0757 498336 ili apata matibabu.
Nyumba iliungua wakati watoto hao wamekaa ndani na wakati huo huo mama wa mtoto alikuwa amekwenda shambani maeneo ya Chitemo wilaya ya mpwapwa.

Wakati mvua inanyesha ghafla nyumba ilibomoka na wakati huohuo walikuwa watoto wawili walikuwa jikoni ndani ya hiyo nyumba.
 
 Baada ya tukio hilo kutokea   ikafanyika uokoaji kwenye nyumba hiyo maeneo ya Chitemo na kufanikisha   kuokoa watoto wote wawili kati ya mmoja aliumia kwa kuangukiwa na udongo wa nyumba hiyo na huyu Ombeni Mbeula aliangukia kwenye moto mpaka kuungua hivi unavyoona kwenye picha lakin hali zao ni salama kwa wote.
Baada ya uokoaji waliamua kumpeleka mtoto huyo kwenye hospitali ya Mima iliyoko Mpwapwa ikashindikana madaktari wakamuagiza aende hospitali ya Mpwapwa hapo hospitalini wakakaa siku mbili katika hospitali ya mpwapwa  na siku ya tatu wakaambiwa waende hospitali ya rufaa iliyoko Dodoma Mjini ambayo ni inajulikana General kwa matibabu zaidi.
Walipofika katika hospitali ya mkoa wa Dodoma wakaanza matibabu lakini uwezo wa kipato cha wazazi wake sio kizuri inahitajika msaada kwa matibabu maana hata dawa hajapatiwa na pesa kwa ajili ya matibabu  haikuweza kupatikana paka sasa
 
Kama umeguswa kutoa ni moyo sio utajiri muokoe mtoto huyu maana hata kula anashindwa mpaka kuona anaona kwa mbali sana.
Mama yake hana simu lakini anatumia simu ya  ndugu yake Ekiria Paskali
 
Kwa yeyote atakayependa kumchangia mtoto huyo atume chochote kwenye namba hii au atumie M- pesa kwenye namba hii 0757 498336

(
PICHA KWA HISANI YA PAMOJAPURE BLOG)

Sunday, February 17, 2013

MAMA SALMA KIKWETE AENDELEA ZA ZIARA YAKE MKOANI LINDI, AGOMA KUFANYA MKUTANO WA NDANI WA CHAMA KATIKA CHUMBA CHA DARASA LA SHULE YA SERIKALI

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Narunyu, Kata ya Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho, Feb 16, 2013.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimiana na watoto wa kijiji cha Narunyu, Kata ya Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho, Feb 16, 2013.
Umati wa wananchi wa Kijiji cha Ng'apa wakimsiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akilipowahutubia mkutano wa hadhara, Feb 16, 2013.
Mkazi wa Kijiji cha Ng'apa wilaya ya Lindi mjini, akionyesha kadi yake ya matibabu ya Huduma ya Kadi uliopo chini ya Bima ya Afya, wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika kijiji hicho, Feb 16, 2013. Mama Salma Kikwete alimpatia fursa ya kuzungumza wakati akihimiza umuhimu wa wananchi kujiunga na mpango huo wa matibabu.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amegoma kushuka katika gari lake, kukataa kwenda kwenye mkutano wa ndani wa Chama Kata ya Tandangongoro, uliokuwa umepangwa na viongozi wa kata hiyo kufanyika katika chumba cha darasa la shule ya msingi ya kijiji cha Ng'apa, mkoani Lindi,  Februari 16, 2013. Hatua hiyo iliwalazimu viongozi kutafuta ukumbi mwingine wa dharura. Mama Salma alisema si sahihi mkutano wa ndani wa Chama cha siasa kufanyika katika chumba cha darasa la shule ya serikali.

DEREVA WA LORI LA MAJI APOKEA KIPIGO CHA MBWA MWIZI BILA HATIA

 Dereva wa Lori la Maji wa Kampuni ya Dolfin yenye maskani yake Mbezi Tang Bovu, jijini Dar es Salaam, ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, akiugulia maumivu baada ya kupigwa na kuumizwa na jamaa wawili waliokuwa na kina dada wawili katika gari ndogo eneo la Mbezi njia inayoingia katika Shule ya Mbezi Beach Sekondari jana usiku. 

Dereva huyu alikuwa akitokea Barabara kubwa akiingia katika njia ndogo inayoelekea Shule ya Sekondari ya Mbezi Beach, na gari ndogo ilikuwa ikitokea katika njia hiyo ndogo na kukutana uso kwa uso na lori hilo, huku watu waliokuwa katika gari hiyo ndogo wakimtaka dereva wa lori kuwapisha wao ili waanze kupita. 

Dereva huyu aliamua kubana kushoto na kuwaachia njia ili wapite, kama picha ya Lori inavyoonyesha chini, lakini jamaa waliokuwa katika gari ndogo waliamua kushuka na kumshusha dereva huyo na kisha kuanza kumshambulia kwa magumi na mawe, huku dereva huyo akitoka nduki na kuacha gari lake, hadi katikati ya barabara inayoelekea Tegeta ikitokea Mwenge, walipomtia mikononi na kuanza kumpiga kama mwizi huku wakitumia mawe kumpigia kama makwenzi, na kumuumiza kama hivi hadi walipofika watu kibao na kuanza kuamulia ugomvi huku wakijua kuwa jamaa huyo ni mwizi huku wengine wakijandaa kuanza kumshambulia. 

Lakini watu hao baada ya kupata stoti kamili ilivyokuwa waliamua kuwageuzia kibao watu hao wakianza kuwasonga kutaka kuwashambulia ndipo walipoamua kudandia gari na kukimbia, huku mmoja kati ya wanawake waliokuwa na jamaa hao, akisikika kumwambia jamaa huyo,

''usirudie kutukana watu waliovaa suti hovyo bila kuwajua watakuua''. 

Gari hiyo wakati ikianza kuondoka eneo hilo huku ikiendeshwa na mwanamama, ilianza kushambuliwa kwa mawe kwa bahati iliwahi kuondoka eneo hilo na kuingia usawa wa Barabara ya Masana na kutokomea.
Watu hao wakidandia gari iliyoanza kutembea ili kutoweka eneo hilo.
Jamaa hao wakianza kuondoka eneo hilo kwa kasi huku gari hiyo ikiendeshwa na Mwanamama.
Lori lililozua kasheshe hilo, ndiyo hili na eneo lenyewe ndo kama hivi linavyoonekana huku magari yakiwa na uwezo wa kupita bila kugusana na lori hilo.
Lori hilo likiwa limeachwa katika eneo la tukio baada ya dereva wake kupewa kipondo huku magari mengine yakipita kama kawaida.

Source:Sufiani Mafoto.blogspot.com

PADRI EVARIST MUSHI WA KANISA KATOLIKI ZANZIBAR AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KICHWANI



Padri Evarist Mushi wa kanisa Katoliki Parokia ya ST. Joseph, Shangani Unguja
 amefariki dunia baada ya kupigwa risasi saa 1.00 asubuhi na kufariki kabla ya kufikishwa hospitalini Mnazi Mmoja visiwani humo.

Padri huyo amepigwa risasi kichwani na kufa papo hapo na watu wasiojulikana wakati  akiwa kwenye gari yake akielekea kuendesha ibada ya saa 3.00 asubuhi ya leo katika kanisa la Mt. Theresia eneo la Mtoni Zanzibar.

Msemaji wa Jeshi Polisi Zanzibar Inspekta Mohamed Mhina amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa padre huyo ameuawa wakati akijiandaa kuingia kanisani akitokea kwenye gari yake ambapo ndipo alipofikwa na umauti huo.

Jeshi la Polisi visiwani humo kupitia kwa Msemaji wake Mkaguzi wa Polisi, Mohamed Mhina limelaani mauaji hayo na kusisitiza kuwa Jeshi limeanza msako mkali ili kuwabaini wauaji hao.
Hili ni tukio la pili kutokea visiwani Zanzibar ambapo tukio la kwanza lilitokea kwa Padri Ambrose Mkenda kupigwa risasi na kujeruhiwa na watu wasiojulikana.

Mungu ailaze roho ya marehemu Padri Evarist Mushi, Amina.

BAADHI YA PICHA ZINAZOONYESHA OFISI YA WEMA SEPETU

Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu zakibongo, Wema Isaac Sepetu ameonesha picha za kwanza za ofisi ya kampuni yake aliyoifungua na kuipa jina la  Endless Fame Films ambayo anatarajia kuizindua hivi karibuni.

Hizi ni baadhi tu za picha zinazoonyesha sehemu mbalimbali za ofisi hiyo ya kisasa.
Ofisi ya Managing Director mwenyewe
Washing room
Hapa ndipo Editor atakapokuwa anafanyia kazi


Wageni tutakuwa tunasubiri hapa

Ofisi ya Sekretari

Kila la Keri na hongera sana Wema Sepetu mungu azidi kukuongoza katika njia ya mafanikio..

BAADA YA KIFO CHA GOLDIE, MUMEWE AJITOKEZA

Pichani juu ni baadhi tu ya picha alizopost mwanaume huyo anaedai kuwa mi mume wa Goldie

Mwanaume wa kizungu aitwaye Andrew Harvey, anayedai kuwa ni mume halali wa  mwanamuziki Goldie Harvey aliyefariki juzi usiku amejitokeza na kupost picha za ndoa na mahaba wakiwa pamoja.

Andrew alishare picha hizo pia kwenye mtandao wa twitter na kuliambia gazeti la Nigeria Entertainment Today kuwa ana admin access za akaunti za mitandao ya kijamii ya marehemu Goldie
.
Hii ni interview exclusive kati ya Andrew na gazeti hilo:

When did you wed her? And were you still married as at when she passed yesterday?


We wed in December 2005 and were very much married when she passed indeed I was talking to her on arrival in Lagos before the fateful event


I see you moved back to England. Do you have another family?


I work in Malaysia, we have a private home in UK, I do not have a second family


Also did you have kids together?

No kids, we were planning this year


There had been speculation for many years that she was married to an ‘oyinbo’ man. But no one could lay hands on anything. Why did you keep it a ‘secret’?

Our private life is nothing to do with work life, there has to be a balance


How did you hear of her death? I found out you last saw her in December?


I was talking to her on arrival in Lagos before the fateful event


How did you meet her? She must have been very young…

I met her at a friend’s leaving party and fell in love straight away, but had to work hard to persuade her I was genuine


So you will be planning to come here for burial rites…


Yes I have applied for visa and shall come next week


But how did you manage the Prezzo drama?

Prezzo was part of BBA game, just like in the movies, there was nothing to fear


But funny it dragged way beyond BBA

It dragged because the media dragged it, other wise it would have died naturally. Prezzo will say anything to get attention


Do you think he fell in love? And did you ever think Susan liked him for a minute…?


People fall in love and it’s not impossible to love more than one person, but there are different levels. She liked him initially, but began to despise him and distanced herself as he tried to use her she complained he was very manipulative


You have direct access to her password? The memories album was posted on her twitter. Or you requested for an admin to post?


I am an official admin. I don’t need any password but my own. It was authorised by Goldie


One last question: so much speculation on cause of death. I see from your facebook timeline that you’ve followed the reports. Have the doctors/family/label told you what the cause of death is?


An autopsy is being carried out and we will await results. The rest is speculation and hearsay


And did she have any medical condition?


She had no medical condition

Is it true she was in India recently?

She was in Malaysia, we spent Christmas together away from prying eyes

What will you miss most about her?

Everything, she was the most beautiful person I ever met, no moment was wasted. Sweet, intelligent, sexy and a magnificent cook!!!!

Monday, February 4, 2013

WATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAVAMIA NYUMBANI KWA MAKAMBA

Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia nyumbani kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba (pichani) kwa lengo la kufanya uhalifu. 
Hata hivyo majambazi hao ambao walimfunga kamba mlinzi wa nyumba hiyo na kuingia ndani, hawakufanikiwa kuiba chochote. Mh. Makamba amesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana wakati yeye akiwa safarini jimboni kwake Bumbuli ila familia yake ilikuwepo nyumbani hapo.
Makamba alisema baada ya majambazi hao kuingia ndani, walimfunga kamba na kumziba mdomo mlinzi.
“Ujambazi huo ulitaka kufanyika nyumbani kwangu Masaki karibu na Ubalozi wa Afrika Kusini, Mimi sikuwepo nyumbani. Walivamia chumbani mke wangu akabonyeza kengele iliyopiga kelele ndio wakakimbia, baada ya majirani kuwasili eneo la tukio, wakatokomea kusikojulikana,” alisema Makamba na kuongeza:
“Waliingia kwenye ofisi yangu ya pale nyumbani na kupekua lakini cha ajabu ni kwamba sebuleni kulikuwa na Ipad na laptop  lakini hawakuvichukua.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu hao walitaka kufanya ujambazi, lakini hawakufanikiwa.
Kamanda Kenyela alisema tukio hilo lilitokea saa 10 alfajiri ya kuamkia jana, lakini majambazi hao hawakufanikiwa kutimiza azima yao.
“Walimfunga kamba mlinzi na kufungua dirisha, kisha kuingia ndani. Lakini hawakufanikiwa kuchukua chochote,” alisema Kamanda Kenyella.
Kamanda Kenyella alieleza kuwa majambazi hao hawakufanikiwa kuiba chochote kwa kuwa wakazi wa eneo hilo, walisikia purukushani na kupiga kelele zilizosababisha watu hao kutokomea.
“Haijulikani walikuwa wangapi kwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyewaona, lakini katika tukio hilo hakuna aliyejeruhiwa,” alisema Kamanda Kenyella.
Alisema baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi Kinondoni, inaendesha msako wa kuwatafuta watu hao ili kuweza kuwatia nguvuni na kuwafikisha mahakamani.

Sunday, February 3, 2013

PICHA KUMI ZA JENGO LA PPF TOWER LILIVYONUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO ASUBUHI YA LEO

Jengo la PPF Tower kabla ya kushika moto
Baada ya kushika moto
Magari ya zimamoto eneo la tukio
Maandalizi ya kuzima moto huo yakianza
 
Mmoja kati ya waokoaji kutoka kikosi cha zimamoto

Kazi ikiendelea
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadick akiwa ameongozana na Kamanda Kova na Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wakiwasili eneo la tukio
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadick akihojiwa na vyombo mbalimbali vya habari

Kamanda Suleiman Kova nae akifunguka kwa vyombo mbalimbali vya habari