Mcheza sinema maarufu duniani kutoka nchini Marekani Deidre Lorenz
atakimbia mbio za kila mwaka za Mount Kilimanjaro Marathon zinazoanza
kutimua vumbi kuanzia tarehe 24 Juni mwaka huu kutoka Moshi Club mjini
Moshi. Mbio hizi zilizoanzishwa na mama Marie France kutoka katika
mji wa Bethesda, Maryland nchini Marekani mwaka 1991 ni mbio
zinazojulikana kama 7 continental Races na zimeshawahi kupata tuzo
mbalimbali za kimataifa.
Ujio wa mcheza sinema huyu aliyecheza
sinema nyingi kama vile Santorini Blue, Perfect Strangers, The Great
Fight, na nyingine nyingi unaiweka Tanzania katika macho ya dunia na
kuwavutia watalii wengi kutoka taifa hili tajiri duniani. Deidre Lorenz
alizaliwa katika jiji la Oregon nchini Marekani lakini akahamia katika
jiji la New York City linalijulikana kama "The Big Apple" nchini
Marekani akiwa na kampuni yake ya kutengeneza sinema inayoitwa Thira
Films LLS.
eidre Lorenz ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu
kugombe tuzo za wacheza sinema maarufu duniani zinazojulikana kama
Grammy Awards. Mcheza sinema huyu ataambatana na Wamarekani wengine
kuja nchini tarehe 21 Juni kukimbia mbio hizi ambazo zimetokea
kuutangaza sana mji wa Moshi tangu mwaka 1991. Lorenz alipatikana katika
bahati nasibu iliyochezwa wakati wa mbio za New York Marathon mwaka
jana.
Naye mwanzilishi wa mbio hizi mama Marie Frances ana
historia ya kuanzisha mbio na matamasha mbalimbali duniani. Alikuwa pia
mwanzilishi wa mbio za Pyramid Marathon nchini Misri pamoja na Miss
Universe Egypt matamasha yaliyojizolea sifa kemkem.Aliombwa kuja
kuanzisha mbio za Marathon nchini Tanzania na balozi wa Tanzania wa
wakati ule nchini Misri.Mbio za Mt. Kilimahjaro Marathon ni moja kati ya
mbio tafauti za marathon zinazifanyika katika mji wa Moshi.
Mount Kilimanjaro Marathon zitaanzia Moshi Club mpaka Rau madukani na
kurudi mara tatu ambazo zitakuwa kilimeta 42. Kutakuwa pia na mbio z
akilometa 21, kilimeta 10 na kilometa 5 kwa watoto. Wakimbiaji
hawahitaji kuwa na ujuzi wa kukimbia watu wote wanaweza kukimbia. |