|
Mange na Devotha a.k.a wake ya wazunguu |
|
Wakifunguka |
|
Mange, Devotha na Super Woman Joyce Kiria |
|
Devotha na Joyce
|
Kuna mambo mengi sana ambayo watu hasa wa jinsia ya kike tukiakaa pamoja huwa tunajadiliana na kila mmoja akielezea uzoefu wake katika mambo mbalimbali aliyopitia katika maisha yake hususan katika suala la mapenzi.
Leo tunaangalia suala la tofauti kati ya walio katika uhusiano wa kimapenzi na wenzetu kutoka mataifa ya ulaya almaarufu kama wazungu na wale walio na uhusiano na waafrika hasa Watanzania.
Kupitia Wanawake Live ya Joyce Kiria utawasikia wake wa wazungu ambao ni Mange Kimambi ambaye pia ni mmiliki wa Blog ya U-turn,Devotha Chuwa aliyewahi kuwa mke wa Marehemu James Dandu ambaye kwa sasa ameolewa na mzungu pia watafunguka kuhusiana na Experience yao katika mahusiano na kukubwa wakizungumzia kuhusu tofauti waliyoiona pale walipokuwa na wabongo na sasa hivi ambapo wapo na wazungu.
Kwa kukudokezea tu ni kwamba tofauti kubwa ambayo wao wameizungumzia ni kuhusu suala la tamaduni, kwa mfano sisi watanzania tuna utamaduni wa kutake Responsibilities kwa ukoo mzima let say shangazi ni mgonjwa utawajibika kumhudumia mpaka au mtoto wa shangazi hana ada ya shule pia utawajibika kumsaidia ili aende shule kitu ambacho ni tofauti kubwa na wenzetu ambao wao wanajali mke/mume na watoto tu, hivyo wanapata Challenges kubwa sana pale wanapokutana na masuala hayo ya kusaidia ndugu.
Kitu cha pili ni kuhusu maisha ya kawaida ya Familia kama mke na mume wenzetu unaambiwa mara nyingi wanafanya mambo yao pamoja, mfano wakitaka kutoka basi wanatoka pamoja, wakati wa chakula kila mmoja muda ukifika basi atakuwa mezani tofauti na sisi ukumuuliza baba ataluambia nyie kuleni tu mimi leo nitachelewa kurudi au katika suala la kutoka mama utapigiwa tu simu kuwa leo nitachelewa kurudi nitakuwa na marafiki zangu sehemu, swali ni kwamba kwa nini msiende wote na mkeo huko kwa marafiki au mna siri gani ambayo mke wako hapaswi kuifahamuuu?
Mengi sana yalizumgumzwa lakini kikubwa ambacho mimi kilinivutia ni kuhusu hiyo tofauti ya kati ya wale walio na uhusiano na hao wazungu na sisi tulio na wabongo wenzetu.. Endelea kuangalia Eatv ting'a namba moja kwa vijana ili uweze kufahamu mengi ambayo yamezungumzwa kwenye hicho kipindi.