Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambaye pia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya New Habari wachapishaji wa magazeti ya
Mtanzania, Dimba, Bingwa na Dimba, Absalom Kibanda amevamiwa na watu
wasiojulikana akiwa ndani ya gari lake wakati akiingia nyumbani kwake
Mbezi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kibanda alivamiwa
majira ya saa sita usiku wa kumkia leo Tar March 6 2013, akitokea kwenye majukumu yake ya
kila siku. Inadaiwa kuwa alichomolewa kwene gari, akapigwa na vitu
vyenye ncha kali kichwani, ametobolewa jicho lake la kushoto pamoja na
kunyofolewa kucha na baadhi ya vidole na hatimaye kutupwa mbali kidogo
kutoka nyumbani kwake.
Baada ya hapo wasamalia wema walijitokeza na
kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambako alipokelewa vizuri na
madaktari na kumpatia tiba ya awali na baadaye kumhamishia Taasisi ya
Tiba ya Mifupa (MOI) ambako mpaka sasa anaendelea na matibabu.
Watu waliomfanyia madhara hayo, hawakuweza kuchukua kitu chochote kwenye gari ambapo kulikuwemo Laptop, simu na nyaraka zingine.
|
No comments:
Post a Comment