Friday, March 22, 2013

DEVOTHA NYARUSI MPIGA GITAA WA KWANZA WA KIKE KALUNDE BAND

Mwanamuziki Devotha Nyarusi amekuwa kivutio kikubwa cha Mashabiki wa Kalunde Band kutokana na umahiri wake katika kazi hasa katika upigaji wa Gitaa.

Mwanamuziki huyo alikonga nyoyo za mashabiki pale alipopanda jukwaani na kuanza kulikung'uta Gitaa katika show yao ya jumapili iliyopita ambapo katika Hotel ya Giraffe.

Akizungumzia kitendo hicho cha mwanadada huyo kukung'uta Gitaa na kufanya kuwa kivutio kwa mashabiki waliokuwa ukumbini hapo na kumshangilia kwa nguvu sana, Rais wa Bendi hiyo Deo Mwanambilimbi alisema umahiri wa mwanadada huyo umewadhihirishia mashabiki kuwa Bendi hiyo inaundwa na wanamuziki wenye vipaji vingi na vya hali ya juu na kuongeza kuwa Bendi hiyo pia inakuza vipaji vilivyojificha na havifahamiki katika ulimwengu wa muziki.

Usikose kusikiliza kipindi cha Afrosunday cha East Africa Radio kinachoruka kila Jumapili saa 1 jioni mpaka saa 4 usiku, wiki hii ili kupata mambo mengi zaidi yanayomhusu mwanadada huyo na Kalunde Band kwa ujumla.

1 comment:

  1. Kija naomba uniwekee picha ya devotha kwa uzuri nimwone akifanya mavituzi. Mimi pia najua piga keyboard, nimevutiwa kusikia hii habari

    ReplyDelete