Friday, July 27, 2012

SHIGONGO AFUNGUKA KUHUSU ISHU YA CHAMELEONE

Mkurugenzi wa kampuni ya Global Publishers Erick Shigongo Pichani juu, amefunguka kuhusu tuhuma zilizokuwa zinamkabili za kushikilia Passport ya mwanamuziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone.Akizungumza na kipindi cha HOTMIX kinachorushwa na EATV jana jioni, Shigongo amesema alifikia hatua hiyo kwa lengo la kumuonyesha Chameleone na wanamuziki wengine kutoka Nchi zingine za Afrika Mashariki kuwa watanzania si wa tu wajinga na wanajua wanachakifanya. Katika mengi aliyoongea pia ameeleza kukerwa kwake na kitendo alichokifanya Chameleone jana cha kwenda katika ubalozi wa Tanzania nchini Uganda na kubamiza mlango na kuongeza kuwa hiyo ilikuwa ni ishu ya biashara ya wao wawili hivyo hakupaswa kulifikisha huko ila walipaswa kumalizana wao wawili.. Hata hivyo Shigongo amekiri kushikilia Passport hiyo na hadi jioni hiyo tayari alikuwa ameshairudisha sehemu husika.

No comments:

Post a Comment