Wednesday, July 18, 2012

WOLPER AJIANDAA KUUPOKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

MUIGIZAJI nyota wa filamu nchini Jacqueline Massawe amesisitiza kwamba amebadili dini na na kuwa Muislam na kwa sasa anajiandaa kwa kuupokea na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza jijini DSM Wolper amesisitiza kwamba yeye kwa hivi sasa ni muislamu na amejitayarisha kufunga na kujizuia kufanya shughuli za kisanii ambazo zitamsababishia kutengua saum yake hivyo kwa kipindi hicho cha muda wa mwezi mmoja atakuwa akijishughulisha na kazi zake zingine.

"Unajua dini ni imani na hii iko ndani ya moyo wangu hivyo nachukizwa kwa kitendo cha baadhi ya ndugu zangu wa karibu kuniita MALAYA na hukumu kwa mambo mbalimbali mimi ndiyo najua nafanya nini katika maisha yangu"alisema.

Aidha amewatupia dongo wale wote wanao mtupia maneno ya kumdhihaki kwamba hatoweza kufunga na kuswali , "Unajua tumepewa miezi 11 ambayo tuko huru kufanya mambo mbalimbali ya starehe za kidunia kwanini nishindwe kujizuia ndani ya mwezi mmoja tu, mimi nasema hivi  nitasali sitakuwa na makucha , manywele  na mambo mbalimbali ambayo hayapendezi katika ibada "

No comments:

Post a Comment