Monday, July 23, 2012

KESI YA LULU YAENDELEA KUPIGWA DANA DANA

Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu  Kanda ya Dar es Salaam Amiri Msumi leo asubuhi  ameahirisha kesi  inayomkabili msanii wa Filamu nchini, Elizabeth Michael(Lulu) anayetuhumiwa kumuua aliyekuwa msanii nyota wa filamu nchini Steven Charles Kanumba Aprili 7,2012.

Akiahirisha kesi hiyo Msajili huyo alisema kutokana na sababu za Jaji anayesikiliza kesi hii katika Mahakama Kuu Jaji Dk. Fauz Twaib kutokuwepo Mahakamani amelazimika kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 20.

"Kwa kuwa Jaji Dk. Fauz Twaib ni mwalimu katika chuo cha  Sheria hivyo yuko katika mitihani naahirisha kesi hii hadi tarehe hiyo niliyoitaja ambapo itakuja kutajwa".

No comments:

Post a Comment