Wednesday, April 17, 2013

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAKUTANA NA WADAU KUTOKA KATIKA NCHI ZILIZOPITIWA NA BONDE LAUFA

Wizara ya Nishati na madini hii leo imefanya mkutano wa siku mbili na wadau mbalimbali kutoka katika Nchi zilizopitiwa na bonde la ufa kwa lengo la kuainisha vivutio vya uwekezaji hasa kwenye sekta ya madini ambapo Tanzania ndiyo wenyeji wa mkutano huo Naibu waziri wa Wizara hiyo bwana. Stephen Masele amesema Sekta ya madini Nchini kwa muda mrefu imekuwa hainufaiki na mapato na kwa kutambua hilo Serikali imefanya jitihada kubwa katika miaka 10 iliyopita kubadilisha na kushughulikia kasoro zote zilizopo katika sekta hiyo.

Aidha Kaimu Kamishna wa madini bw. Ally Samaje amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya madini, Mtanzania anatakiwa kuwa na hisa ya zaidi ya asilimia 25 katika mradi wa kununua na kuuza madini ambapo mgeni hatakiwi kuwa na hisa ya zaidi ya asilimia 75.



Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya ukaguzi wa madini bw. Paul Masanja amesema, Tanzania imekusanya zaidi ya Tshs Bilioni 480 kutokana na kodi ya mapato ya migodi mikubwa tangu kuanza kwa ukaguzi wa kodi katika migodi hiyo miaka mitatu iliyopita.

Bw.  Masanja ameongeza kuwa makusanyo hayo ni kutoka katika migodi mikubwa mitatu ambayo ni Mgodi wa Geita uliolipa Bil. 299, Mgodi wa golden Pride uliolipa bil. 90.4 na Mgodi wa Tulawaka uliolipa Bil. 77.4

No comments:

Post a Comment