Monday, April 22, 2013

CHOKI KUZIKATAA TENA TUZO ZA KILI, AAHIDI KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WAKIMUINGIZA KWA NGUVU KWENYE KINYANG'ANYIRO

Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo (pichani) kwa mara nyingine tena, ametangaza kutoshiriki katika Tuzo za muziki za Kili (Kilimanjaro Music Awards) kwa kile alichodai kuwa hana imani na Tuzo hizo na kuongeza kuwa.zina mapungufu mengi.
Akiongea na blog hii Choki alisema kuwa mwaka jana alikataa kushiriki katika mchakato huo lakini Bendi yake iliingizwa kwa nguvu nae alienda BASATA kuomba mwaka unaofuatwa Bendi yake isiingizwe kabisa kwa sababu Tuzo hizo zina mapungufu makubwa sana.

"Hizi tuzo zina mapungufu makubwa sana huwezi kuwaweka Diamond, Ally Choki, Gurumo na Mzee Yusuph kwenye uimbaji bora au unamuweka Linah, Luiza Mbutu na Khadija Kopa wakati wanafanya muziki tofauti, kwa staili hii kuna watu hawatendewi haki.

Choki ameongeza kuwa mwaka huu atawafikisha mahakamani waandaaji endapo watamuingiza kwenye kinyang'anyiro hicho bila ridhaa yake wakati ameshatangaza kuwa hazihitaji Tuzo hizo mpaka pale zitakapofanyiwa marekebisho. 

No comments:

Post a Comment