Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya ukaguzi wa madini bw. Paul Masanja amesema, Tanzania imekusanya zaidi ya Tshs Bilioni 480 kutokana na kodi ya mapato ya migodi mikubwa tangu kuanza kwa ukaguzi wa kodi katika migodi hiyo miaka mitatu iliyopita.
Bw. Masanja ameongeza kuwa makusanyo hayo ni kutoka katika migodi mikubwa mitatu ambayo ni Mgodi wa Geita uliolipa Bil. 299, Mgodi wa golden Pride uliolipa bil. 90.4 na Mgodi wa Tulawaka uliolipa Bil. 77.4
|