Tuesday, February 7, 2012

TOA KWA MOYO KUOKOA MAISHA YA MAMA ANAYEUGUA FISTULA

Ofisa mkuu wa masoko na mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba akiimba nyimbo mbalimbali na baadhi ya akina mama wanaotibiwa ugonjwa wa Fistula katika Hospitali ya CCBRT, mara baada ya kuzindua kampeni ya MOYO inayolenga kuhamasisha jamii kuchangia fedha kwa ajili ya wanawake wenye uganjwa huo hapa nchini, kuchangia kwa njia ya M-PESA Tuma kwenda namba 200500 na kwa njia ya SMS tuma ujumbe mfupi usemao MOYO kwenda namba 15599
Baadhi ya akina mama wanaotibiwa ugonjwa wa Fistula katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar Es Salaam wakiimba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya MOYO .
Mkazi wa jijini Mbeya Stella Nzyemba aliyetibiwa ugonjwa wa Fistula,akielezea jinsi alivyokata tamaa ya maisha baada ya kuugua ugonjwa huo kwenye Hafla ya uzinduzi wa kampeni ya MOYO.
                                                              Kufahamu zaidi ingia hapa


No comments:

Post a Comment