Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Bongo LADY JAYDEE (Pichani) kwa kushirikiana na Bendi yake ya Machozi, leo wanatarajia kuipongeza Timu ya Yanga kwa ushindi wa Kombe la Kagame walioutwaa mwishoni mwa wiki
Msemaji wa Timu hiyo LOUIS SENDEU (Pichani)amesema wachezaji hao wakiongozana na viongozi wa Timu hiyo pamoja na wageni waalikwa watajumuika na LADY JAYDEE pamoja na Machozi Band katika Mgahawa unaomilikiwa na msanii huyo unaofahamika kama NYUMBANI LOUNGE kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kufurahia ubingwa huo kwa pamoja
Mashabiki wa timu ya YANGA wakiwa wamemzunguka Kapteni wa Timu hiyo SHADRACK NSAJIGWA siku waliyotwaa ubingwa huo katika uwanja wa TAIFA jijini DSM.
No comments:
Post a Comment