Thursday, August 29, 2013

Mapacha waliozaliwa wameungana Zenji, wafanikiwa kutenganishwa

Jopo la Madaktari Bingwa Saba wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa ya hospitali hiyo (Moi), wamefanikiwa kuwatenganisha pacha waliokuwa wameungana kiwiliwili.

Iliwalazimu mabingwa hao kutumia saa nne kufanikisha upasuaji huo. Mmoja wa watoto hao waliotenganishwa, amelazwa kwenye Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU) Taasisi ya Mifupa Moi wakati kiwiliwili kingine kilifariki.(P.T)

Jopo la madaktari waliofanikisha upasuaji huo ni; bingwa mstaafu wa watoto ambaye aliitwa maalumu kwa kazi hiyo, Petronila Ngiloi, Dk Robert Mhina (mifupa) na Profesa Karim Manji aliyekuwa akifuatilia kwa karibu mapigo ya moyo.

Wengine ni Dk Karima Khalid aliyekuwa akiratibu dawa ya usingizi, Dk Hamis Shaaban (ubongo na uti wa mgongo), Dk Zaitun Bokhary (bingwa upasuaji watoto) na Dk Nyangasa (moyo na mishipa ya fahamu).

Akizungumza baada ya upasuaji huo, Dk Shaaban alisema walimfanyia vipimo mtoto ambaye hakuwa amekamilika na kugundulika kuwa hakuwa amekamilika viungo vyote achilia mbali kutokuwa na kichwa na macho pia hakuwa na moyo, figo, tumbo, maini ila alikuwa na uti wa mgongo.

"Uti wa mgongo ulikuwepo na ndio uliokuwa umeshikana na mwenzake na kuna mshipa mmoja wa fahamu ulikuwa unafanya kazi ndio maana alikuwa ukimgusa anachezesha mguu."

Alisema kinachoratibiwa kwa sasa ni kuangalia dawa ya usingizi aliyopewa mtoto ambaye anaendelea kupumua na kwamba ndani ya saa 24, dawa ya usingizi waliyomuwekea mtoto huyo itakuwa imeisha na ataanza kunyonya kama kawaida.

Upasuaji
Kazi ya upasuaji huo ilianza saa mbili asubuhi kwa mtoto huyo wa jinsi ya kike aliyetimia kuchukuliwa vipimo mbalimbali ikiwemo CT Scan, MRI, Ultra sound na vingine vingi kabla ya upasuaji kamili kuanza saa tano asubuhi.

Dk Shaaban alisema ni mara ya kwanza kwa Moi kufanya upasuaji wa aina ile na kwamba mara nyingi wamekuwa wakifanya upasuaji wa watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa pamoja na mgongo wazi ambao tatizo hilo linasababishwa na upungufu wa madini ya folic acid.

Kabla ya upasuaji kuanza, mama wa mtoto huyo Pili Hija (24) alitumia muda wa nusu saa kufanya maombi maalumu ya kumwombea mtoto wake kisha kuwaruhusu madaktari kuendelea na upasuaji huo.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuruhusiwa kumwona mtoto wake, Hija alisema: "Ninamshukuru Mungu kwa yote na nazidi kumwomba amjalie mwanangu apone kabisa, nawashukuru na nitazidi kuwaombea madaktari wanaomtibu mwanangu."

Alijifungulia nyumbani Agosti 18 maeneo ya Jang'ombe, Zanzibar watoto pacha walioungana mmoja akiwa amekamilika viungo vyote na mwingine akiwa na kiwiliwili.

Kahaba ala kichapo baada ya kujiuza karibu na msikiti

Kahaba  mmoja   alijikuta akiambulia kichapo kikali toka kwa vijana wa kiislamu baada ya kunaswa akijiuza karibu na msikiti wao..

 Kutokana na kukerwa na vitendo hivyo, vijana hao wanaofanya ibada katika msikiti huo, waliamua  kuwatafuta vijana wa ulinzi shirikishi na kuwapa kazi hiyo ya kuwakamata na kuwacharaza bakora kisha kuwapeleka katika kituo hicho cha polisi.

“Tumeamua kuwakamata na kuwacharaza bakora, hawana ustaarabu wala busara hawa, wanakojoa na kutupa kondomu  hovyo, “ alisikika mmoja wa vijana hao.
Mmoja wa vijana hao aliyekuwa akisimamia kwa karibu zoezi hilo, aliwaambia waandishi wetu kuwa wameamua kufanya hivyo na litakuwa zoezi endelevu kutokana na wanawake hao kutokuwa wasikivu kwani kila wanapoambiwa juu ya kukaa mbali na nyumba hiyo ya ibada hawasikii.

Alisema kuwa siku moja wanawake hao walimtoa udhu muumini mmoja ambaye alikuwa akienda kuswali alfajiri baada ya kumshika na kusababisha akose kuhudhuria swala siku hiyo.


Hata hivyo, wakati mahojiano yanaendelea, mmoja wa askari waliokuwa zamu aliamuru mwanamke huyo aingizwe lokapu kusubiri kesho yake aunganishwe na wenzake kisha wapelekwe mahakamani.

Habari zilizotufikia  ni kwamba baada ya kufikishwa mahakamani na kukutwa na kosa la uzururaji, wakahukumiwa kifungo cha miezi sita jela au faini ya shilingi elfu hamsini ambapo walilipa kiasi hicho na bado wanaendelea na biashara hiyo maeneo hayo.



Wednesday, August 28, 2013

Hemedy PHD aendelea vizuri

Muigizaji Hemedy Suleiman ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongofleva amefunguka kuwa anaendelea vizuri baada ya kupata ajali mbaya ya gari na gari hilo kudaiwa kuharibika.

 Hemedy alikuwa akimsindikiza Gerry Wa Rhymes ambaye pia ni msanii maarufu nyumbani kwake Sinza na kupata ajali baada ya kugonga kalivati. Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Hemedy ameandika

"Namshukuru mungu naendelea vizuri baada ya kupata ajali mbaya iliyonikuta..ahsanteni kwa dua zenu, kifua tu ndiyo kimeumia na mkono"

Get well soon Hemedy

Friday, August 23, 2013

Mwakyembe, magufuli na Lukuvi wakumbwa na tuhuma nzito

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge.

Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012.

Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni.

“Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha hizi zilipunguzwa kiasi cha Sh95 bilioni na kupelekwa Wizara ya Uchukuzi, zilibakia Sh252.975bilioni katika kifungu hicho lakini kuna bilioni 100 zimetumika visivyo,” alisema Zitto, ambaye pia ni Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema).

Alisema katika majumuisho ya Bajeti ya wizara hiyo, Dk Magufuli na Dk Mwakyembe wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Lukuvi walitoa maelezo yasiyo ya kweli bungeni kuhusu fedha.

Alikariri maneno yaliyorekodiwa kwenye Hansard ya Bunge yaliyosemwa na viongozi hao watatu.

“Tunaomba fedha Sh252 bilioni kwa ajili ya kuanzia kazi za ujenzi wa barabara,” Zitto alisema akikariri maneno ya Dk Magufuli wakati anawasilisha bajeti.

“Fedha hizi zitachangia miradi ya wafadhili,” haya yalikuwa maneno ya Dk Mwakyembe wakati akifanya majumuisho.

“Hizi ni fedha kwa ajili ya counterpart fund,” alimkariri Lukuvi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.

Zitto alisema CAG alihoji mwaka huu kuhusu matumizi ya fedha hizo na alitoa taarifa akidai kuwa fedha hizo zilikuwa miradi hewa na kasma kivuli.

Zitto alisema kuwa Dk Magufuli na Katibu Mkuu wake walipohojiwa walidai kutumia fedha hizo kulipa madeni.

“Kwa nini mlidanganya Bunge? Mliomba fedha za kuanza miradi maalumu. Hamkuomba fedha za madeni. Kwa nini mliunda kasma kivuli na kuifuta baada ya pesa kulipwa?” Zitto alimhoji Balozi Mrango.

Katika majibu yake, Balozi Mrango alisema kwa nia njema, fedha hizo zilitumika kuwalipa makandarasi waliokuwa wamechachamaa, huku baadhi yao wakisisitiza kusitisha kuendelea na miradi. Hivyo wakalazimika kuomba fedha kwa njia hiyo ili miradi kuendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Zitto hakuridhishwa na majibu hayo akisema hapakuwa na haja ya kutumia fedha hizo kuwalipa makandarasi wakati kulikuwa na kasma yao ya awali. Alisema kama kulikuwa na haja hiyo, wizara isingeita mradi rasmi.

“Jambo hili siyo sahihi hata kidogo kulidanganya Bunge na hadi sasa wewe na waziri wako hamuonyeshi kukubali kosa hili, hata Waziri Lukuvi naye alisisitiza bungeni kwamba fedha hizo zinaombwa ili kutekeleza mradi maalumu lakini sasa imebainika sivyo, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge tutawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ili wahojiwe nao wajieleze kwa kulidanganya,” alisema Zitto.

Pia kamati hiyo imeitaka wizara hiyo kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu matumizi ya Sh100 bilioni zilizotumika kinyume na maombi yaliyowasilishwa kwenye Bajeti ya mwaka huo wa fedha.

CAG ameshauri madeni yote ambayo Wizara ya Ujenzi inadaiwa yaorodheshwe ili yawe wazi kuepuka migongano katika matumizi ya fedha.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Lukuvi alisema haelewi chochote na kusisitiza kuwa akipata taarifa rasmi za Kamati ya PAC, atatoa ufafanuzi.



Halmashauri zinavyotafuna mabilioni

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAACc), imeeleza namna mamilioni ya fedha za Serikali zinavyoibwa kutoka Hazina kupitia halmashauri za wilaya huku Ilala ikitajwa kuongoza kwa ufisadi huo.

Mwenyekiti wa LAAC, Rajab Mbarouk Mohammed aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba Hazina imekuwa ikipeleka fedha kwenye halmashauri zikiwa zimezidi na kwamba kiasi kinachozidi hakirudishwi badala yake huliwa.

Alisema kamati hiyo imefanya uchunguzi kwenye halmashauri 43 na kubaini kwamba mtindo huo ndiyo unaotumika kuiba fedha za Serikali.

“Mwaka 2011/12 kiasi cha Sh1.5 bilioni zilipelekwa zikiwa zimezidi kwenye halmashauri hizo lakini hazikurudishwa Hazina kama inavyoonyesha kwenye ripoti ya CAG.

Alisema kati ya kiasi hicho, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilipewa ziada ya Sh213 milioni ikifuatiwa na Geita iliyopewa Sh129 milioni.

“Fedha hizo za mishahara zilipelekwa kwenye halmashauri hizo na Hazina kimakosa zikiwa zimezidi lakini watendaji wa hawakuzirudisha kama wanavyotakiwa kisheria badala yake zikayeyuka,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa uchunguzi huo pia ulibaini kwamba katika halmashauri hizo 43 kiasi cha Sh693 milioni hulipwa mishahara hewa ambayo wafanyakazi wake walishakufa na wengine kustaafu.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ililipa mishahara hewa yenye thamani ya Sh79.4 milioni ikifuatiwa na Ukerewe iliyolipa Sh57.5 milioni.

Kwa upande wa fedha za miradi ya maendeleo, mwaka 2011/12, Hazina ilipeleka katika Halmashauri ya Mbarali, Mbeya Sh724 milioni kwa ajili ya Mradi wa Maendeleo ya Elimu Sekondari wakati mradi huo ulikuwa ukihitaji Sh70 milioni tu.

“Kiasi cha Sh654 milioni zilipelekwa kimakosa na Hazina lakini badala ya kurudishwa zilitumiwa katika mazingira ya kutatanisha,” alisema.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ilipelekewa ziada ya Sh500 milioni na Mvomero ilipewa Sh85 milioni. “Kuna mtandao mkubwa wa Hazina na halmashauri ambao ukiachwa utaendelea kupoteza fedha nyingi za walipakodi,” alisema.

Hatimaye GK kurudi kwenye gemu rasmi


Hatimaye baada ya kimya cha muda mrefu Mwanzilishi wa kundi la East Coast Team (ECT) “Crazy Gk” aliyetamba na nyimbo kama sauti ya Manka, miko kumi ya rap, sister sister na simba wa afrika anamipango ya kurudi kwenye game la bongo flava.

Msanii huyo aliyepotea kwa muda mwingi akiwa masomoni sasa anataka kurudi tena kwenye game na atazindua wimbo wake mpya wiki ijayo kupitia radio station tofauti tofauti hapa Tz.

Tusubiri tuone ukimya wake uko vipi, Je ataweza kubamba na kukubalika kama ilivyokuwa hapo mwanzo au watoto wadogo wa sasa watampiga bao...karibu kakka mkubwa!!!

Ujenzi wa bweni la wanafunzi albino waanza chini ya Miss TZ Brigitte



MREMBO wa Tanzania, Brigitte Alfred ameonyesha mfano wa kuigwa nchini katika tasnia hiyo baada ya kuanza ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (albino) katika wilaya ya Shinyanga wanaoishi katika shule maalum ya Buhangija. Tayari mrembo ameweka jiwe la msingi na kupandisha ukuta sambamba na kukabidhi mabati 200 kwa ajili ya kujengea paa la bweni hilo la wavulana lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 50.

Makabidhiano hayo yalifanywa na mrembo huyo kwa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi, afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga Honoratha Ruhumbika na walimu wa shule hiyo wakiongozwa na mwalimu mkuu, Peter Ajali.

Briggite alisema kuwa ameamua kutimiza ahadi yake aliyoitoa mwezi Aprili mwaka huu alipotembelea Shinyanga kwa kazi za jamii na kuona changamoto za watoto wanaosoma katika shule hiyo.

Alisema kuwa mpango huo upo katika mpango wa Miss Tanzania ujulikano kwa jina la Urembo wenye malengo maalum (Beauty with Purpose) nay eye kuamua kufanya kwa vitendo.

“Ni faraja kwangu kuona kuwa ninatimiza ahadi yangu, nawashukuru wote walionisaidia ikiwa pamoja na familia yangu, na ninaomba wengine wanisaidie kwani badi kuna changamoto nyingi katika ujenzi na kazi za jamii kwa ujumla,” alisema Brigitte.

Alisema kuwa amepania kuweka historia katika fani hiyo kwani anaamini ujenzi au jingo hilo litakuwa kumbukumbu kubwa kwake tena kwa vizazi na vizazi.

Brigitte pia aliwataka wanafunzi hao kutokata tamaa hata kwa wale wasiokuwa karibu na familia zao na kwamba wamtegemee zaidi Mwenyezi Mungu kwa kuwa yeye ndiye mfariji kwa wanyonge huku akiwahimiza kuzingatia zaidi elimu kwani ndiyo msingi wa maisha yao.

 “Nilipata msukumo wa kuisaidia shule hii hususani katika ujenzi wa bweni hilo kutokana na ujio wake wa mwezi Aprili mwaka huu shuleni hapo na kujionea adha wanayopata watoto hao kutokana na msongamano mkubwa mabwenini,” alisema.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi alimpongeza Brigitte kwa moyo huo wa kujitolea na kuwataka warembo wengine kuiga mfano wake. Nyamubi alisema kuwa alichokifanya Brigitte ni jambo la kukumbukwa nan i msaada mkubwa kwa jamii hasa kwa watu wenye ulemabu wa ngozi.

Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba wazazi wa watoto hao kuwa na tabia ya kuwatembelea watoto wao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwachuku wakati wa likizo. Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Peter Ajali alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo la msongamano mabwenini kwani kuna jumla ya watoto 247 huku mabweni yaliyopo yana uwezo wa kukaa watoto 148 tu.

Thursday, August 22, 2013

Tundaman akimbia uchi, kisa deni la laki 4


Msanii Tundaman amejikuta akiambulia aibu ya mwaka baada ya kujitosa nusu uchi mtaani akiwakwepa askari polisi ambao walivamia kwake leo asubuhi kwa lengo la kumkamata....

Chanzo cha Tunda man kusakwa na polisi ni deni la sh. laki nane ambazo alikopa mwanzoni mwa mwaka huu kwa mwanadada mmoja ( jina kapuni)....

Taarifa zinadai kwamba, baada ya kupewa hela hiyo, Tunda man aligeuka kisima cha matusi ya nguoni kwa mrembo huyo. Kila akipigiwa simu alikuwa hapokei, na akipokea ni matusi ya nguoni.....

Baada ya hali hiyo, mwana dada huyo aliamua kulifikisha swala lake polisi ambapo Tundaman alikamatwa. Akiwa mikononi mwa polisi, msanii huyo aliomba apewe nafasi ya kulilipa deni lake kwa awamu tatu kuanzia tarehe 12/8/2013

Baada tarehe hiyo, Tundaman hakuweza kulipa kiasi chochote na wala hakutoa ushirikiano wowote, hali iliyomfanya mwanadada huyo arudi kuripoti polisi....

Polisi walianza jitihada za kumsaka ambapo leo majira ya saa nne asubuhi walivamia kwake ( Tabata Savana ) kwa lengo la kumkamata.....

Bahati nzuri au mbaya, Tundaman alifanikiwa kuwatoroka polisi akiwa na bukta tu ( kwa mujibu wa mashuhuda) na kutokomea kusikojulikana...

Nyota wa 'Prison Break' ajitangaza rasmi kuwa ni shoga (GAY)



Star wa “Prison Break”,  Wentworth Miller  a.k.a Michael Scofield, amejitangaza kuwa yeye ni “Gay” (shoga), katika barua ya wazi aliyoiandika kwenda kwa Directoe wa St. Petersburg International Film Festival (tamasha la filamu la kimataifa la St. Petersburg)

Muigizaji huyo (41) ameandika barua hiyo kukataa mualiko uliokuwa ukimtaka kuhudhuria tamasha hilo linalofanyika nchini kwao Russia na kwa mara ya kwanza kupitia barua hiyo amejitangaza kuwa yeye ni “Gay” (shoga).
“Asante kwa ukarimu wa mualiko wako, nikiwa kama mtu ambaye amefurahia kutembelea Russia kwa miaka ya nyuma na naweza pia kudai shahada ya asili ya kirusi, ningefurahi kusema ndio, hata hivyo nikiwa kama shoga lazima nikatae”. amesema Miller

Miller akaendelea kusema … nasumbuliwa sana na tabia ya sasa dhidi ya na jinsi wanavyochukuliwa mashoga na wanawake  na serikali ya Urusi.


“hali hii haikubaliki kabisa, na mimi siwezi kwa dhamira nzuri kushiriki katika tukio la kusherehekea linaloandaliwa (wenyeji) na nchi ambayo watu kama mimi kwa mfumo uliopo wananyimwa haki zao za msingi za kuishi na kupenda kwa uwazi”


akamalizia kwa kusema.. kama hali hii itarekebishwa, nitakuwa huru kufanya uchaguzi tofauti.



Matako makubwa ya mchumba wa mtu yamponza na kufumaniwa

Katika hali ya kustaajabisha na pengine ikaingia kwenye kumbukumbu ya maisha yake, mtu mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Sebastiani mkazi wa Kurasini jijini Dar, jana Jumatano alijikuta kwenye aibu kubwa baada ya kufumaniwa na mchumba wa swahiba yake wa kufa na kuzikana.

Tukio hilo ambalo lilitokea mishale ya saa 2 usiku kwenye gesti ya Green Pau iliyopo maeneo hayo ya Kurasini ilitokana na mchumba wa jamaa (binti) kumtonya jamaa yake kwamba kuna mtu anamtaka kimapenzi.

"Baada ya mchumbaangu kuniambia hayo niliangalia ile namba na kugundua mtu aliyekuwa kimtaka mchumba wangu ni rafiki yangu wa zamani sana tena ni wakufa na kuzikana," alisema jamaa huyo kwa masikitiko. Alisema kutokana na jamaa huyo kutaka kutembea na mchumba wake na yeye aliamua kumfanyia umafia wa kumuumbua mbele ya jamii ili iwe fundisho kwa wengine.

"Nilikaa nikatafakari sana maana jamaa alikuwa akimtumia mchumbaangu meseji ambazo siwezi kuzisoma hapa maana ni aibu lakini kubwa alikuwa akimtaka mchumba wangu kinyume na maumbile akidai amejaaliwa sana," alieleza jamaa huyo mbele ya umati wa watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.

Taarifa zinaeleza kwamba baada ya hapo mipango ya kumfumania jaama huyo ilianza kuandaliwa na takribani mara mbili walipopanga kukutana na mchumba huyo wa mtu alichomoa kwa madai kwamba alikuwa akizidiwa na kazi.

 "Kama mara mbili walipanga kukutana lakini dakika za mwisho jamaa alichomoa kwa madai ya kuzidiwa na kazi lakini leo za mwizi zimetimia," alidai jamaa huyo baada ya kumfumania rafiki yake huyo akiwa uchi wa mnyama na mchumba wake kwenye gesti hiyo chumba namba 04.Dakika chache baadae alifika mkewe wa mfumaniwa na kutokana na tukio hilo alisema hana la kusema zaidi ya kumshukuru mungu kwa aibu aliyoipata toka kwa mumewe huyo wa ndoa.

"Kiukweli sina la kusema hii ni aibu kubwa sana...mume wangu kila siku anadai hapa pesa za matumizi nauza mkaa ndio tule na watoto kumbe ndio mambo aliyokuwa anayafanya, nashukuru sana," alisema mke huyo mbele ya waandishi wa habari.

Hadi mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio, aliwaacha wakiwa ndani ya chumba wakiendelea kuombana msamaha.

Wednesday, August 21, 2013

Muumini na Waziri Sonyo wachapana LIVE

BAADA ya kuvuliwa urais 'Kocha wa Dunia sasa wanamuziki wawili nguli, Waziri Sinyo na Muumin Mwinjuma, Rais wa zamani wa bendi ya Victoria Sound, wamezichapa kavu kavu live wakati wa  mazoezi ya bendi yao yaliyofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam, jana.

Katika kichapo hicho, inadaiwa kuwa Sonyo nusura amchome Muumini kisu, hivyo kuzua hofu katika patashika hilo la aina yake linaloendelea kuonyesha mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki hao ndani ya bendi ya Victoria Sound.

Akizungumza muda mchache baada ya sakata hilo, Muumini alisema alishangaa kujikuta yupo chini na Sonyo akiwa ameshatoa kisu kutaka kumjeruhi.

Muda mchache baadaye Muumini aliandika kwenye mtandao wa kijamii akielezea tukio hilo alilodai ni la aina yake huku akitumia lugha kali za kuudhi dhidi ya Sonyo.

“Leo ndio nimedhihirisha huyu (TUSI LIMEHIFADHIWA) ni kweli amenikuta nimekaa tena pembeni na tahadhali zote ila alivyokuja kwangu kunivamia sikumkawiza nikampa ngumi 3 takatifu zilizolenga uso wake ndio akaona kumbe huyu mzima akatoa kisu mfuko wa kulia watu wakamuwahi kumshika, lakini wakati nakwepa kisu nilianguka, na kama sio George Gama angekuwa ameshanijeruhi au kuniua kabisa, ngoja nimfunze adabu nampeleka mahakamani ili iwe fundisho na kwa hili sina msalie mtume hivi jimwili lote la Sonyo Bado anamshikia mwanaume mwenzie Kisu na amshukuru, Janurry aliyenipakata ningempukutisha meno kwa ngumi maana alikuwa kama kuku mgonjwa hakurusha hata ngumi," mwisho wa kunukuu meseji ya Muumini.

Kupigana kwa wanamuziki hao ni mwendelezo wa mgogoro mzito uliokuwapo kwa bendi hiyo baada ya uongozi pia kumuondoa katika nafasi ya urais Muumini na kumpa Kassim Muhumba, huku pia Sonyo akienguliwa katika nafasi yake ya kiongozi wa shoo.

Je ni kweli Kocha wa dunia atajiweka pembeni na kuachana na muziki kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni, kama alivyoesema kuwa iwapo Victoria Sound itakufa ama kuondoka katika bendi hiyo, basi ataachana na muziki na matukio haya inawezekana mwanamuziki huyo ameanza kujilaumu kwa kauli hizo TATA.

Mjue binadamu mwenye kilo 610



Mfalme wa Saudi Arabia, ameingilia kati mpango wa kumsaidia Raia wa nchi hiyo, Khalid bin Mohsen Shaari ambaye ndiye binadamu mnene na mzito zaidi duniani akiwa na uzito wa kilogram 610, katika mchakato wa kumtibu na kumrudisha katika hali nzuri zaidi.

Kutokana na unene, ukubwa na uzito wake, Khalid hawezi kutembea wala kusogea mwenyewe bila msaada wa kifaa maalum cha kumbeba akiwa katika kitanda chake, na cha ajabu zaidi, Ni mshkaji mdogo tu ambaye umri wake ni kati ya miaka 18 na 20.

 Kwa mujibu wa rekodi za Guiness, Manuel Uribe kutoka Mexico ndiye aliyekuwa akishikilia rekodi ya mtu mzito na mnene zaidi duniani ambapo alikuwa na uzito wa kilo560, Na baada ya kuonekana na kuingizwa katika matibabu, kwa sasa amepungua na kufikia uzito wa kilo 444.

Mfalme Abdullah tayari ametoa amri kuwa Khalid kuhamishwa huko Riyadh kwaajili ya mchakato wa matibabu yake.

Tuesday, August 20, 2013

Young D aja na 'Kijukuu'

Msanii wa Bongo fleva Young Dar es Salaam (Young D) anatarajia kuachia kichupa chake cha Kijukuu wiki ijayo.

Kichupa cha ‘Kijukuu’ kimefanyiwa na director anaekuja kwa kasi hapa Tzee’ Nisher’ kwa uwezo wake mkubwa anaouonesha katika baadhi video zilizotoka,na Location iliyotumika katika video ya ‘Kijukuu’ ni ya jiji la Dar es Salaam.

Young D alifunguka kuhusiana na video yake “ Kichupa changu nimekifanya kwa Nisher na location imetumika ya mkoa wa Dar es Salaam na nimeamua kufanyia hapa Dar kutokana na kuwepo kwa material mengi, so fans wangu wategemee kichupa kikali na next week watakiona kwenye luninga zao”

Kemikali yaunguza vijana 12 huko Handeni

VIJANA 12 wa kijiji cha Manga kilichopo kata ya Mkata wilayani hapa, wameanza kunyofoka nyama kutokana na madai ya kubeba magunia yenye kemikali baada ya lori lililokuwa limebeba mzigo huo, kupinduka katika eneo la dajani la kitongoji cha Tengwe kijijini.

Vijana hao wamepata athari hizo baada ya kupewa kibarua cha muda mfupi wa kubeba maguni yaliyokuwa na uzito wa kilo 25 kuyafaulisha kwenye gari jingine na kulipwa ujira wa sh. 95,000 ambazo waligawana sh. 11,500 kila mmoja baada ya kumaliza kazi hiyo.

Ofisa Tarafa ya Mazingara Bw Hashim Msagati alisema kuwa tukio hilo limetokea Julai 26 mwaka huu majira ya saa 11:00 jioni katika eneo hilo baada ya lori lenye namba za usajili T 787 CBT lililokuwa na tela lenye namba T 101 BTB kupinduka kisha watu waliokuwa kwenye gari hilo, kuwapa kazi vijana hao kubeba mizigo hiyo.

Alisema lori linadaiwa kumilikiwa na kiwanda cha soda cha Bonite kilichopo mjini Moshi, lilipata ajali hiyo iliyothibitishwa na polisi wa kituo cha Mkata, lilikuwa likitokea Jijini Dar es salaam kwenda mkoani Kilimanjaro, likiwa limebeba mifuko yenye kemikali hizo.

Wakizungumza na gazeti hili, wakiwa nyumbani kwao katika kijiji hicho cha Manga, mmoja ya waathirika hao Bw. Said Omari alisema walipata kazi hiyo kutoka kwa mtu mmoja aliyekuwa na asili ya Kihindi kupakia mifuko hiyo bila kuelezwa kwamba kilichomo ndani yake ni madawa makali
.
Aliwataja wenzake waliokuwa pamoja ni Omari Bahorela, Khatib Juma, kassim Bakari, Hamis Chilo, Ramadhani Rajab, Ramadhani Mbelwa na Omari Mbuji kutoka katika mji wa Manga na Lazaro Jackson, Aweso Mussa, Mkombozi Mussa na Mohamedi Shabani waliotokea kitongoji cha Tengwe.

Alisema baada ya kufika kwenye eneo hilo, walianza kubeba mizigo hiyo na kuipakia kwenye gari jingine lakini ghafla mwezao mmoja Kasimu alianza kuanguka chini akawa hawezi kusimama baada ya madawa hayo kuanza kumuunguza miguuni na kwenye shingo hatua ambayo walianza kuogopa kuendelea na zoezi hilo.
“Mwenzetu alipokuwa ameanguka chini akawa hawezi kuinuka huku akilia miguu kumchoma kwa ndani na huku akishindwa kuinuka pale chini, tulianza kuogopa tukamwagia maji tukazidisha maumivu, tulikataa kuendelea na zoezi lile lakini yule Mhindi akasema hapana endeleeni mifuko iliyobaki, vinginevyo hatatulipa,” alisema Bw Said.

Alisema hata hivyo, waliendelea kubeba na walipomaliza wakalipwa fedha hiyo ingawa walikuwa wamekubaliana ujira wa sh. 100,000 wakapewa sh. 95,000, lakini mwenzao yule hakuweza kutembea hadi wakambeba pamoja na Mhindi huyo kumrudisha nyumbani kwao kisha wakaondoka kuendelea na safari.
Bw Said alisema kesho yake walianza kunyofoka nyama kila mmoja aliyebeba mizigo hiyo na ngozi kuwa nyeupe huku wakipata maumivu kwenye uti wa mgongo na maeneo mengine ya miili yao hatua ambayo wanashindwa kupata matibabu sahihi kutokana na kukosa fedha.

Akizungumzia zaidi tukio hilo Bw. Msagati alisema kuwa wamepeleka taarifa hizo kwa viongozi wa wilaya ili waweze kuchukua hatua ya kuwatafuta waliohusika kwa ajili ya kuwasaidia matibabu vijana hao na kusafisha eneo lililopata ajali hiyo amba[po wanahofu kwamba endapo mvua itanyesha, inaweza kusombwa na kuingia katika visima vya maji na kuleta madhara makubwa kwa jamii.

Mkuu wa wilaya ya Handeni, Bw Muhingo Rweyemamu alisema atafika katika kijiji hicho kuwatembelea vijana hao kisha kuona eneo lililopata ajali kabla ya kuchukua hatua nyingine.

Monday, August 19, 2013

Nasoro Mangunga atajwa kuhusika na madawa ya kulevya na Mwakyembe

Waziri wa uchukuzi Prof. Harrison Mwakyembe amemtaja mshukiwa mmoja wa dawa za kulevya aitaye Nassoro Mangunga, lakini mshukiwa huyu pamoja na picha zake alishaandikwa na gazeti la SANI katika toleo lake la Agosti 7-9, 2013 (toleo la 1042) pamoja na namna alivyosafirisha mzigo pamoja na akina Masogange.

Hii ndiyo taarifa yao:

Unaweza kukimbia lakini huwezi kujificha. Msemo huu unaonekana kutimia kwa kijana anayedaiwa kuambatana na watuhumiwa wa dawa za kulevya waliokamatwa Julai 5 mwaka huu nchini Afrika Kusini, Agness Gerald 'Masogange' (25) na Melisa Edward (24), kunaswa na gazeti hili.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, wasichana hao, Masogange na Melisa walisafiri ndege moja na kijana anayejulikana kwa jina la Nassoro Mangunga wakitoka Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini, wakisafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA), yenye namba SA 189.

Wakiwa katika ndege hiyo Mangunga, Agness na Melisa walikaa kwenye viti vilivyo jirani kabisa huku Mangunga akiwa katikati yao, kwani Agness alikaa kiti namba 23B, Mangunga alikaa kiti namba 23D na Melisa alikaa kiti namba 23A.

Mangunga ambaye ni rafiki mkubwa wa wanamuziki wa Bongo Flava, Rashidi Abdallah Makwiro 'Chid Benz', Mgaza Pembe 'M2theP' na Albert Keneth Mangweha 'Mangwair', wakati akisafiri na mabinti hao walikuwa na jumla ya mabegi tisa kama kumbukumbu za nyaraka za shirika hilo la ndege zinavyoainisha.
Licha ya nyaraka za kusafirishia mabegi hayo kuonesha jina la Agness Gerald ambaye ni mpenzi wa Mangunga tangu mwanzoni mwa mwaka jana, kuwa ndiye aliyelipia mabegi hayo, ila kwenye sehemu ya anuani ya waraka pepe, imeandikwa ya Mangunga (inahifadhiwa) ya tovuti ya Gmail.

Aidha, mabegi hayo, yalikuwa na kilo 150 za dawa za kulevya lakini kila mmoja alitakiwa kusa
firi na kifurushi cha kilo ishirini kama mzigo wa mkononi ambao husafiri bila malipo, hivyo watatu hao kwa pamoja walikuwa na kilo sitini wote kwa pamoja, hivyi kubaki kilo 90 ambazo walizozilipia Dola za Marekani 94 badala ya Dola 450.

Mangunga ambaye licha ya kuishi zaidi nchini Afrika Kusini, lakini pia ni mkazi wa maeneo ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Agness na Melisa, walikamatwa Julai 5, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Thambo, Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya Sh bilioni 6.8 za Kitanzania, na walipotiwa mbaroni, walikuwa na mabegi sita tu kati ya tisa waliyokuwa nayo wakati wanapanda ndege jijini Dar es Salaam.

Inasemekana mabegi hayo matatu yaliondoka na Mangunga na kutokomea kusikojulikana, jambo linalolifanya Sani kuzamia zaidi ili kuweka mezani timu nzima inayohusika na mzigo huo

Friday, August 16, 2013

Mwakyembe apambana na wauza madawa

JUHUDI za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe za kupambana na dawa za kulevya nchini Tanzana zimeanza kuzaa matunda baada ya jana akiwa katika ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Julius Nyerere kunaswa kijana akijaribu kupita na dawa za kulevya katika uwanja huo.

Kwa kuonyesha kuoneshwa kukerwa na tabia hizo, Dk. Mwakyembe amempiga picha kijana huyo ambaye ni rasta na picha yake itasambazwa maeneo tofauti, huku kesi yake ikiendelea ya kupatikana na madawa hayo ya kulevya.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe alimtaja kijana aliyekamatwa jana kuwa ni Leonard Jeremiah Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroin akitaka kusafiri nazo,huku misokoto ya bangi 34 akiwa ameficha kwenye begi lake.

Alisema kijana huyo mwenye nywele za kusokota (rasta) alinaswa na mtambo wa kukagua mzigo baada ya wakaguzi kuushuku mzigo wake hivyo kuamuru ukaguliwe ndipo alipokutwa na madawa hayo haramu akijaribu kusafiri nayo kwa ndege.

Alisema kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukutwa na dawa hizo haramu. Alisema kwa kile kuoneshwa kukerwa na vitendo hivyo na kuamua kwa dhati kupambana navyo wamempiga picha kijana huyo na picha zake zitasambazwa maeneo mbalimbali ili aonekane na umma kujua watua ambao wamekuwa wakilichafua taifa nje na ndani kutokana na biashara hizo haramu.

Dk. Mwakyembe amesema atahakikisha anafuatilia kesi ya kijana huyo hadi itakapoishia ili uona hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na vitendo hivyo kukomeshwa. Alisema maofisa wakaguzi wa mizigo wawili (wote wasichana) ambao walimnasa kijana huyo watazawadiwa na kupandishwa daraja kutokana na kazi nzuri waliyoifanya.

“Jana tu baada ya ukaguzi wenzetu ambao wanaona kama tunafanya mzaha jana tena wakapitisha mzigo wa madawa ya kulevya kiwanja cha ndege cha Dar es Salaam, kwa sababu vijana wetu sasa wameamka na hawataki mchezo wakamkamata kijana huyo…,” alisema.

“Picha yake itasambazwa kila sehemu…sidhani kama tunahitaji upelelezi kwa sababu tumekukamata na dawa za kulevya. Mimi na viongozi wangu kupitisha dawa za kulevya akikisha kuuhakikisha.

Alisema kijana huyo alikamatwa majira ya saa mbili na nusu usiku akiwa anasafiri kwenda nchini Italia kwa kutumia ndege ya kampuni ya Swissair. Alisema kwa sasa kila atakayekamatwa na dawa za kulevya picha yake itasambazwa maeneo mbalimbali ya nchi ili watu hao wajulikane.

Alisema kwa sasa taratibu zinafanywa ili kuhakikisha mizigo ya abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi kuingia Tanzania nao mizigo ikaguliwe ili kuwabaini wanaoingiza bidhaa hiyo haramu ichini pia. Aliongeza zoezi hilo litafanyika katika viwanja vya ndege na bandarini kwa kila mizigo inapowasili.

Alisema lengo ni kuhakikisha viwanja vya ndege vinakuwa salama na kuacha kutumika vibaya na baadhi ya watu, jambo ambalo limeendelea kulichafua taifa. Alisem kiwanja cha Dar es Salaam ni kizuri na kina vifaa vya usalama vya kutosha ila mapungufu yaliyopo ni kwa baadhi ya wafanyakazi ambao wanatumia vibaya madaraka yao.

Dk. Mwakyembe ameahidi kuwataja na kuweka picha zao hadharani watu ambao wanajihusisha na madawa hayo ya kulevya. Amesema wanatarajia kutaja majina ya Watanzania ambao hivi karibuni walinaswa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo. Alisema Watanzania wengine wamekamatwa Hong Kong wakihusishwa na dawa hizo na wanafuatilia pia picha na majina yao yatawekwa hadharani muda wowote.

Ujio mpya wa Johari

Ikiwa imepita miezi kama sio miaka kadhaa tangu mwanadada Blandina Chagula a.k.a Johari apotee machoni mwa watazamaji wa muvi za kibongo, ameamua kurudi tena kwenye uigizaji wa muvi hizo kivingine.

“Ijapokuwa watu walikuwa hawanioni lakini kazi za RJ company zilikuwa zinaendelea kutoka na zote nimeshiriki kikamilifu utengenezwaji wake na kwa namna nyingine ni kupisha tu vipaji vipya vipate kuonekana na sio kila siku ni Johari tu.” Johari alifunguka.

Kwa sasa Johari anashinda location kila siku na hadi sasa tayari amekamilisha muvi mbili ndani ya RJ ziitwazo Bad Luck ambayo amecheza bila Ray kuhusika kwa mara ya kwanza na nyingine ni Long Huck aliyocheza na Ray huku nyingine zikiwa zinamkosesha usingizi location kila siku.

“Labda niseme kwamba kwa mara ya kwanza, nimeshiriki filamu nje ya RJ na watu wengine kabisa kwa kunialika kwenye muvi zao huku nikishirikiana na chipukizi wengi.” Aliongeza Johari

Filamu alizoshirikishwa ni pamoja na Mke mchafu, Masumbuko nk. kitu ambacho hapo kabla hakuwahi kukifanya. Welcome again lady…!!!

Thursday, August 15, 2013

Majangili waitisha serikali

SERIKALI imesema mtandao wa majangili wanaoua tembo mkubwa wenye watu walio na uwezo kifedha ambapo wapo ndani na nje ya nchi .

Siri hiyo ilifichuliwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Mali Asili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Alisema tayari Serikali ina majina ya mtandao unaojihusisha na biashara ya ujangili wa meno ya tembo na baadhi yao wapo pia wafanyabiashara wakubwa waliopo ndani na nje ya nchi.

"Tayari majina tunayo ya mtandao wa watu wanaojishughulisha na ujangili wa meno ya tembo huu ni mkubwa ambao una pesa nyingi, hauna tofauti na ule wa dawa za kulevya,"alisema

Alisema sio kwamba wameshindwa kufanya kazi bali wanaendelea kupata taarifa na wameandaa operesheni hai itakayosaka wale wote ambao wanahusika na ujangili huo.

Aliongeza kuwa wanaendelea kufuatilia nchi inayonunua meno hayo ambapo nchi zilizopo Bara la Asia ni miongoni mwa zinazo husikana biashara hiyo.Ali sema siorahisi ku shinda vita hiyo kwa kutumia vyombo vya habari.

 "Mnajua hii ni vita kubwa na ni waambie kuwa vita hii huwezi kushinda kwa kutumia vyombo vya habari, hivyo Watanzania kuwe ni na amani na tunajitahidi kuhakikisha tunamaliza tatizo hili,"alisema.

Katika hatua nyingine,alisema mfumo wademokrasia uliopo unachangia kurudisha nyuma jitihada mbalimbali zinazofanywa, kwani watu wakikamatwa na kupelekwa mahakamani kesho yake wanaonekana mtaani.

 Alisema wanaobainika kufanya biashara hiyo ya ujangili hata Polisi wamo na wengine wameshafukuzwa kazi na wengine kusimamishwa, hivyo hizo zote ni jitihada za Wizara yake.Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo John Lembei alisema kuwa kamati yake imeiomba Serikali kuondoa kodi ya asilimia tatu ambayo ilipitishwa na bunge kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya utalii na asilimia kumi ambayo yalikuwa yanawasilishwa Serikalini kwani inachangia kuondoa huduma za jamii zilizokuwa zikitolewa kwenye jamii inayozunguka hifadhi hizo.

Alisema kamati imeomba serikali kama kweli wanataka kuendeleza sekta ya utalii basi kodi hiyo ifutwe vinginevyo hifadhi hazitakuwa salama na ujangili utaongezeka kwa kiasi kikubwa.

"Hifadhi hizi za TANAPA na ngorongoro ilikuwa miradi ya kusaidia jamii inayowazunguka kwa kuwajengea shule, hospitali, maji, pamoja na huduma zinginezo hivyo kutokana na bunge kupitisha kodi hiyo wameondoa huduma hizo,"alisema Lembei.

Wednesday, August 14, 2013

Muuaji wa mfanyabiashara Erasto Msuya wa Arusha akamwatwa


Polisi wamefanikiwa kumtia mbaroni mfanyabiashara tajiri wa madini ya Tanzanite huko Mirerani anayetajwa kuwa ndiye aliyepanga na kukodi watu waliomuua bilionea Erasto Msuya.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zimedai kuwa mfanyabiashara huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana na juzi alikuwa akihojiwa na makachero.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mfanyabiashara huyo ndiye aliyetoa fedha za kununulia pikipiki mbili zilizotumika katika mpango huo na pia alitoa fedha kwa ajili ya kununua simu mpya na laini mpya.

“Tumewakamata watu wametupa mwanga mzuri na huyo mfanyabiashara ndiye aliyetoa fedha za kununua pikipiki na siku moja kabla ya tukio zilihifadhiwa nyumbani kwake,” alidokeza polisi mmoja.

Habari hizo zimedai kuwa polisi pia imewahoji mawakala wa kampuni za simu ambao walitumiwa kusajili laini mpya za simu zilizotumika kumpigia marehemu na kutumika kupanga mauaji hayo.

Pikipiki hizo mbili, zilinunuliwa siku moja kabla ya tukio zikahifadhiwa nyumbani kwa mfanyabiashara huyo hadi siku iliyofuata ambapo aliwakabidhi wauaji na zote zimekamatwa.

Mahojiano kati ya mfanyabiashara huyo na Polisi yamekuwa yakifanyika kwa siri na katika kituo cha polisi (jina tunalo) na kwamba mambo ni mazuri.


lakini hakitatajwa jina lake.

Chanzo cha mashabiki kutaka kumponda mawe Diamond huko Kenya hi hiki!

Baada ya mashabiki kurusha makopo stejini kisa Diamond kuchelewa kupanda hizi ndio sababu zinazosemekana za kushelewa kwake kupanda

Umati wa watu waliohudhuria show ya Platnum wakirusha makopo stejini baada ya Diamond kuchelewa kupanda hizi ndio sababu zilitajwa kupelekea kuchelewa kwake.

mtandao wa kenya Ghafla umeripoti kuwa Diamond alichelewa kwasababu alikua akijifanya "Diva" pale ambapo kwa maksudi alijichelewesha Tanzania na hivyo kuchelewa ndege kuelekea Kenya.

Baada ya kuchelewa ndege Diamond alidai aletewe ndege binafsi (Private Jet) na National Media Group (NMG) ambapo iliwabidi wafanye hivyo.

Mda mfupi baada ya Diamond kutua Mombasa aligoma ku-check in katika hoteli aliyoandaliwa (Mombasa Beach Hotel)  ambapo ndipo show ilipokuwa ikifanyika na kusisitiza kuchukuliwa presidential  suite White Sands Hotel ambayo iliwagharim mkwanja mrefu NMG.

Baada ya mahitaji yake kukamilishwa ndio Diamond alikubali kupanda stage, na kukitifua mbaya stejini  kwa show ya ukweli na perfomance ya hatari na kuwaachia watu wakiwa na historia isiyofutika leo wala kesho, show ambayo inayoweza kuelezeka kama ni ya ki legendary, Mashabiki walitulia na kuimba nyimbo zake mwanzo mwisho..

Msanii Bongo movie achomwa kisu cha usoni

MSANII wa filamu Bongo, Hamisa Moshi hivi karibuni amechomwa kisu usoni akiwa maeneo ya nyumbani kwao Ilala, Bungoni jijini Dar huku akiwahusisha wasanii wenzake na unyama huo.

Akizungumzia sakata hilo Hamisa alisema siku ya tukio alipigiwa simu na kijana aitwaye John akimtaka wakutane ili wazungumzie dili la kazi.

“Aliponipigia simu akaniambia tukutane, tukakutana maeneo ya Ilala. Yeye alikuwa kwenye gari, akaniambia niingie. Kwa hofu nikasita, mara likaja gari likiwa na wasichana watatu
ambao walinianzishia vurugu na mmoja akanichoma kisu.

“Nilipiga kelele za mwizi ndipo watu walipokuja na kutaka kuwapiga wakidhani ni wezi, nikawazuia ila nakawaambia tuwapeleke polisi ambako niliwafungulia jalada la kesi lenye namba ILA/RB/2952/2013 KUJERUHI.

“Baada ya hapo nilipewa PF3 kabla ya kwenda Hospitali ya Amana na kushonwa nyuzi nane,” alisema Hamisa.

Hata hivyo, msanii huyo alishangazwa na maelezo yaliyotolewa polisi na watuhumiwa hao waliotajwa kwa majina ya Merry, Tiko, Thecla na Mile kwamba eti walikuwa wakimdai shilingi milioni moja, kitu ambacho si kweli.

Tuesday, August 13, 2013

Jeneza la bilionea Msuya, lafunguliwa kwa rimoti


Mazishi ya kifahari yanaandaliwa na familia ya marehemu Erasto Msuya, huku ikielezwa kuwa jeneza litakalotumika kubeba mwili wake linafunguka kwa kutumia ‘rimoti’.

Msuya aliyeuawa wiki iliyopita, anazikwa leo huku familia ikitangaza kutokulipiza kisasi kwa waliohusika, badala yake wamemwachia Mungu.

Kinachovutia katika msiba huo ni jeneza lililobeba mwili wa mfanyabiashara huyo lililoagizwa Nairobi, la aina yake huku likifunguliwa kwa kutumia ‘rimoti’.

Jeneza hilo lililoagizwa kutoka Kampuni ya Montezuma & Monalisa Funeral Home, linafunguliwa kwa kubonyeza kifaa maalumu hata mhusika anapokuwa mbali.

Hali hiyo ilionekana kuwaacha na mshangao maelfu ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wakati wa ibada iliyofanyika nyumbani kwake, Kwa Iddi, wilayani Arumeru.

Mfanyabiashara huyo aliyeuawa kwa kumiminiwa risasi zaidi ya 20 na watu wasiojulikana, anazikwa leo nyumbani kwao eneo la Kairo Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.

Kaka wa marehemu, Israel Msuya, alisema jana kuwa mazishi hayo yatafanyika makaburi ya familia ya mzee Elisaria Msuya ‘Kikaango’, baba wa marehemu Erasto.

Kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya mazishi hayo inayoongozwa na kaka mkubwa wa familia ya Msuya, Gady, zaidi ya Sh100 milioni zimepangwa kugharimia shughuli za maombolezo na mazishi.

Jeneza na gari maalumu la kubebea mwili wa marehemu yameagizwa kutoka Kampuni ya Montezuma & Monalisa Funeral Home ya Nairobi, Kenya kwa gharama ya Sh8 milioni.

Chakula, vinywaji, mapambo na magari ya kukodishwa kutoka Arusha kwenda Mirerani na kurudi yanatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh80 milioni.

Katika hatua nyingine, polisi mkoani Arusha imeendelea kuwahoji wafanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro, wakidaiwa kuhusika na kifo hicho.

Habari zilizopatikana jana zinadai mfanyabiashara mmoja kijana ambaye aliibuka ghafla kuwa tajiri mkubwa kutokana na biashara ya madini ya Tanzanite, anashikiliwa Arusha kwa mahojiano.

Jana, kwenye viunga vya Mji wa Mirerani watu walitangaziwa kuwa mfanyabiashara huyo, alikuwa anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na kifo hicho.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, hakupatikana mara moja kuelezea suala hilo kwani simu yake ilipopigwa ilikuwa haipatikani.

Marehemu ameacha mke na watoto wanne, huku akiacha rasilimali nyingi ikiwamo jumba la kifahari lililopo Sakina kwa Idd, hoteli maarufu za SG Resort na Mezza Luna zilizopo Arusha.

Mjue Fiq Q vizuri

1.TOKA FID Q ATOE WIMBO WA FID Q.COM MWAKA 2003 AMEKUWA AKICHAGULIWA KUWANIA TUZO YA 'MSANII BORA WA HIP HOP' KATIKA TUZO ZA TANZANIA LAKINI HAJAWAHI KUSHINDA TUZO HIYO MPAKA LEO.

2.FID Q ALIANZA KUANDIKA MISTARI YAKE MWENYEWE AKIWA DARASA LA NNE NAKUPIGA BEAT DARASANI KATIKA SHULE YA MSINGI NYAHABUNGUHUKO MWANZA.

3.FID Q AKIWA SHULE PIA ALIKUWA ANACHEZA KIKAPU.

4.KAMA FID Q ASINGEKUWA MSANII,ALIWAHI KUSEMA KUWA ANGEKUWA WAKILI KWASABABU DARASANI ALIKUWA VIZURI.

5.FID Q ALIWAHI KUITAJA ALBUM YA MSANII PROFESA JAY 'MACHOZI JASHO NA DAMU' KAMA ALBUM AMBAO ANAIHESHIMU NA ITAENDELEA KUWA CLASSIC KWAKE.

6.FID Q NI MSHABIKI WA KUNDI LA KWANZA UNIT MPAKA LEO.

7.KABLA YA KUTOA NGOMA YAKE MWENYWE ILIYOMTAMBULISHA FID Q VIZURI 'HUYU NA YULE', FID Q ALIWAHI KUWEPO NDANI YA KUNDI LILILOKUWA LINAENDA KWA JINA LA 'MACHIZI WA HATARI'.

8.FID Q ALISEMA MSANII WA KUIMBA AMBAYE ALITOKEA KUMKUBALI NA KUMUELEWA NA AMBAYE YEYE ANAAMINI KUWA HAKUNA MSANII MWENYE UWEZO WA KUIMBA KAMA YEYE NI NURUELY.

9.WIMBO WA 'CHAGUA MOJA' AWALI FID Q ALIKUWA AREKODI NA PRODUZA CASTRO AMBAYE NDO ALIFANYA NAE FID Q.COM,LAKINI KUTOKANA NA TUKIO LILITOKEA KATI YA CASTRO NA MAREHEMU STEVE2K,ILIMBIDI 'FID Q' AKAFANYE 'CHAGUA MOJA' KWA P FUNKY MAJANI'.

10.FID Q ANA ALBUM 2, 'VINA MWANZO KATI NA MWISHO' NA 'PROPAGANDA'.

11.FID Q NI BABA WA MTOTO MMOJA WA KIUME ANAYEENDA KWA JINA LA 'FEISAL'.

12.FID Q NI MSANII WA KWANZA WA HIP HOP TANZANIA KUWA NA KIPINDI CHAKE MWENYEWE CHA TV KILICHOKUWA KIKIRUKA EATV,KUHUSU HIP HOP 'FID STYLE'.

13.FID Q NDIYE ALIYEANDIKA WIMBO WA 'ZERO' ULIOSHINDA TUZO YA CHANNEL O MWAKA 2008.WIMBO ULIKUWA WA WITNES WAKILISHA NA PIA FID Q ALISHIRIKISHWA.

Monday, August 12, 2013

Mfanyabiashara Arusha amlawiti mfanyakazi wake

Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, (jina linahifadhiwa) ameingia katika kashfa nzito baada ya kurekodi mkanda wa video ukimwonyesha akimlawiti mfanyakazi wake wa dukani.

Kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu kimeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu anayepatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mtu mwingine kinyume cha maumbile.

Video za mfanyabiashara huyo ambazo zimekuwa gumzo zimekuwa zikisambazwa kupitia mitandao ya simu hususan Whatsapp na nyingine zikiuzwa katika maduka yaliyopo Stendi Kuu ya Mabasi Moshi.

Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo kijana anayemiliki maduka matatu Stendi Kuu ya Mabasi, alirekodi video hizo kwa siri bila mfanyakazi wake huyo kujua na kuihifadhi kwenye kompyuta.

Haijajulikana ni nani aliyeingia katika kompyuta hiyo na kunakili picha hizo ambazo moja ina sekunde 45 na nyingine inayomuonyesha akimlawiti mfanyakazi wake huyo ikiwa na muda wa dakika nane.

Habari za uhakika zilizopatikana zimedai kuwa kwa sasa mfanyabiashara huyo pamoja na mwanamke huyo wametoroka na hawajulikani walipo baada ya kubaini wanasakwa na polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Robert Boaz alipoulizwa jana alisema ingawa hajaona video hizo, lakini kufanya mapenzi kinyume cha maumbile ni kosa la jinai hivyo watamtafuta mfanyabiashara huyo.

Kamanda Boaz alisema polisi wanamsaka ili ahojiwe kuhusiana na video na vitendo hivyo alivyoiita ni vichafu na kwamba kimsingi anatakiwa kujisalimisha mwenyewe ili kumaliza mambo.

Alitoa wito kwa jamii kufuata maadili ya dini zote ambapo zinawataka binadamu waishi kwa kumtii Mwenyezi Mungu.

Sunday, August 11, 2013

FEZA kaiaga BBA

Feza Kessy, mtanzania pekee aliyekuwa amebaki katika jumba la Big Brother Africa, amekuwa mshiriki wa 20 kutolewa katika jumba hilo usiku wa leo.

Kwa week 11 zilizopita, Feza aliishi maisha ya kipekee sana ambayo ilikuwa ni aidha unampenda ama unamchukia na si vinginevyo.

Baada tu ya mtangazaji IK kutangaza kuwa Feza ndiye anayeaga mashindano hayo, Feza aliwakumbatia washiriki wengine na kuondoka kuelekea stejini ambako alipofika tu, IK alimtupia swali la kama bado “anampenda Oneal..?” na ndipo Feza akajibu “ndio” bila kusita japo pia alionyesha kuwepo kwa hali fulani ya kutokuaminiana kati yake na Oneal hasa baada ya kukiri kwamba siku za mwanzo Oneal alivutiwa zaidi na mshiriki mwenzie Cleo.

Feza ameondoka na matumaini ya watanzania kuipepea bendera ya ushindi hasa ikizingatiwa kwamba mshiriki mwenzie Nando alitolewa katika mashindano hayo takribani wiki mbili zilizopita kwa kuvunja sheria za Big Brother.

Aliyekuwa sukari wa Feza katika mjengo huo, Oneal, aliyaaga mashindano hayo wiki iliyopita kwa kupata kura chache ukilinganisha na washiriki wenzie waliokuwa kikaangoni ambao ni Feza na Bimp.

Friday, August 9, 2013

Vigogo wawili wabanwa kwa kumtuma Masogange

HABARI zilizochimbuliwa kwa undani zinadai kuwa tayari vigogo wawili waishio nchini wamebanwa na Jeshi la Polisi Tanzania wakituhumiwa kumtuma Masogange kupeleka madawa ya
kulevya nchini Afrika Kusini.

Agnes Gerald 'Masogange'  Kwa mujibu wa habari hizo, vigogo hao (majina tunayo) walidakwa wiki iliyopita kila mmoja kwa wakati wake na kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jijini Dar ambako walihojiwa kwa saa sita.

“Hawa vigogo walikamatwa wiki iliyopita na kuhojiwa kwa masaa sita, waliachiwa lakini waliambiwa wakihitajika tena wataitwa,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo kikaongeza kuwa, licha ya kuhojiwa na kuruhusiwa kuondoka, vigogo hao, mmoja alinyang’anywa ‘paspoti’ yake huku mwingine akaunti zake za benki zikifungwa kwa muda usiojulikana.

Habari zinasema kuwa, kigogo ambaye akaunti zake zimefungwa amekuwa akihaha kila kukicha kuhakikisha zinafunguliwa kwa sababu hana njia nyingine ya kuingiza kipato.

Juzi, Ijumaa liliwasiliana na Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ili kujua uhakika wa madai hayo ambapo alisema:

“Sisi (polisi) tumekuwa tukifanya mambo yetu kwa siri kubwa, si rahisi kusema. Tukisema kunakuwa na ugumu kwa sababu mnaandika kwenye magazeti, matokeo yake uchunguzi unavurugika.

“Mfano wale wasichana (akina Masogange) waliokamatwa Afrika Kusini wamekuwa wagumu kuwataja waliowatuma kwa sababu hao waliowatuma ndiyo wanaowategemea kuwawekea dhamana.”


Agnes Gerald na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park nchini humo wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8

Watalii waliomwagiwa tindikali Zenji warejea UK

Wanawake wawili waingereza waliochomwa kwa Acid nchini Zanzibar wanatarajiwa kuwasili nchini Uingereza baadaye leo

Kirstie Trup na Katie Gee, wote wenye umri wa miaka 18 kutoka London, walipelekwa hospitalini nchini Tanzania baada ya kushambuliwa Mashariki mwa kisiwa hicho.

Inaaminika kuwa walitoka Tanzania kuelekea Uingereza Alhamisi usiku.

Mama za wasichana hao, Rochelle Trup na Nicky Gee, walielezea kughadhabishwa mno na shambulizi hilo ambalo sababu yake haiwezi kujulikana na ambalo halikuchochewa kivyovyote. Walishambuliwa na wanaume wawili waliokuwa kwenye pikipiki.

Polisi walisema kuwa walirushiwa ACID kwenye nyuso zao, kifuani na kwenye mikono yao walipokuwa wanatembea mjini .

Mwandishi wa BBC anasema kuwa waliowashambulia walitoroka na polisi hawajui kwa nini wanawake hao walilengwa.

Mama za wasichana hao walisema kwenye taarifa yao kuwa walighadhabishwa mno na shambulizi hilo na hawaelewi kwa nini wasichana hao walishambuliwa ili hali walikwenda Zanzibar kwa nia njema.

''Tunashukuru kwa wale wanaotaka kujua kinachoendelea lakini tungeomba vyombo vya habari vituwache kwa sasa hadi tutakapokutana na watoto wetu,'' walisema akina mama hao.

Wasichana hao walikuwa wamekaa Zanzibar kwa muda wa wiki mbili ingawa walitarajiwa kuwa huko kwa wiki tatu, kupitia kwa kampuni ya usafiri ya i-to-i Travel, ambayo ilisema inafanya kila iwezalo kuwarejesha nyumbani Uingereza.

Kari Korhonen, mkurugenzi mwenza wa kampuni ambayo wasichana hao walikuwa wanafanyia kazi, alisema kuwa hali yao si mbaya ikizingatiwa athari za Acid kwa mwili na visa ambavyo vimewahi kushuhudiwa vya kuchomwa kwa ACID.

Msemaji mwingine aliongeza kuwa wasichana hao walikuwa njiani kuelekea kwa maankuli ya jioni wakati wa shambulizi hilo.

Thursday, August 8, 2013

Papii Kocha amwaga chozi baada ya kuwaona Wema na Kajala


MASTAA wawili wanaotamba katika filamu za Kibongo, Kajala Masanja na Wema Isaac Sepetu hivi karibuni walifunga safari hadi Gereza la Ukonga jijini Dar kwa ajili ya kumuona Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ anayetumikia kifungo cha maisha gerezani humo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mara baada ya mastaa hao kufika na kuonana na Papii Kocha ambaye anatumikia kifungo cha maisha sambamba na baba yake Nguza Viking ‘Babu Seya’ inadaiwa kuwa Papii aliangua kilio cha nguvu.

“Nimewaona Kajala na Wema Gerezani Ukonga,wameenda kumuona Papii Kocha. Sasa nimeamini kuwa Kajala amejifunza mengi kutokana na kuwekwa mahabusu kipindi kile,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.

Baada ya kupata taarifa hizo Risasi Mchanganyiko liliwatafuta mastaa hao ili kutaka kujua undani wa safari yao hiyo.

Gazeti hili liliwapigia simu na kuzungumza na Kajala baada ya namba ya Wema kutokuwa hewani.

“Kweli mimi na Wema tulienda gerezani kumuona Papii ilikuwa ni safari ya majonzi sana, Papii aliangua kilio sana alipotuona,” alisema kwa kifupi Kajala na kukataa kusema kilichojiri zaidi.

Wednesday, August 7, 2013

BSS sasa kurushwa TBC

Madamu Rita wa Epiq Bongo Star Search kaelezea sababu zilizofanya kipindi chake hicho kuanza kurushwa na TBC1 jumapili hiina isiwe ITV kama ilivyokuwa kipindi cha nyumaKatika mtandao wa FaceBook ktk Page yake ameandika maneno yafuatayo..

""Baada ya kusoma maoni yenu, ningependa kufafanua sababu mbili za kurusha Epiq Bongo Star Search 2013 kupitia kituo cha Televisheni cha TBC1.

Kwanza kabisa ni sababu za kibiashara ndio zimepelekea kipindi cha EBSS kurushwa kupitia TBC1 na sababu ya pili ni kwamba baada ya kwenda kidigitali, TBC1 sasa inapatikana kwenye ving'amuzi karibia vyote vikiwemo Star Times, DSTV na Zuku.

Nashukuru sana kwa maoni yenu mlioyatoa na mmesikika. Nawatakieni siku njema!""

Mgosi atinga Mtibwa

Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Daring Club Motema Pembe ya Congo DRC ametua kwenye timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani Morogoro kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mgosi amesema tayari wamemalizana kila kitu na Mtibwa na msimu ujao atakuwa na wakali hao wanaonolewa na kocha Meck Maxime.

Amesema ametazama mechi mbalimbali za Mtibwa walizocheza za kujiandaa na msimu anaamini kuwa atangára na klabu hiyo kwa mara nyingine na kuwatesa makipa wa timu pinzani.

Mgosi amewahi kuchezea kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kwa nyakati kadhaa,amewahi kucheza Simba alikosajiliwa kutoka kwa maafande wa JKT Ruvu na kabla ya kutua Mtibwa alicheza kwenye ligi kuu ya Congo DRC akiwa na DC Motema Pembe.

Hivi karibuni Mgosi alikuwa nchini China alikocheza mashindano maalumu ya mataifa ya Africa na kuibuka kuwa kinara wa kuzifumania nyavu kwa mara ya pili mfululizo kwenye michezo ambayo Tanzania iliibuka na ubingwa.

Friday, August 2, 2013

Rose Ndauka chupuchupu kuachwa

BAADA ya msanii wa filamu nchini Rose Ndauka kuripotiwa kufumaniwa akiingia gesti na
msanii chipukizi wa muziki wa bongo fleva Nassoro Ayoub 'Dogo Nasry' huku akiwa amevaa baibui kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani,  mumewake mtaarajiwa Maliki Bandawe 'Chiwaman' amjia juu msanii huyo kwa madai ya kumchafua mpenzi wake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Chiwaman aliweka wazi kuwa msanii huyo Nasry ambaye alimuomba Rose aweze kushiriki kwenye video yake, walishindwa kufikia maamuzi kutokana na kiwango cha malipo kuwa madogo, na badala yake msanii huyo alimuomba wapige picha kama ukumbusho.

Alisema kuwa kitendo hicho cha kupiga picha na msanii huyo wakati wapo katika mazungumzo ya awali ya kukubaliana malipo ndizo picha alizotumia msanii huyo na kudai kuwa alikuwa naye nyumba ya wageni kitendo ambacho si cha kweli.

"Hawa wasanii wachanga wanatafuta umaarufu vibaya kwa kuwachafua watu, ilikuwa amemuomba Rose ashiriki kwenye video yake na ndipo walipokutana kwa ajili ya mazungumzo hayo na alikuwa na mdogo wangu sasa hapo masuala ya gesti yametokea wapi" alisema Maliki.

Aliongezea kuwa "kama nilikuwa sijui hicho kitu na kwa jinsi mambo yalivyokuwa ningeweza kumuacha mchumba wangu ninayempenda kwa dhati, ila msanii huyo alichokifanya siyo jambo sahihi, kwani alimuomba apige naye picha na Rose alikubali huku bila kujua nia yake ".

Maliki alisema kuwa huyo msanii anatafuta umaarufu kwa kuchafua majina ya watu wengine, kitu ambacho hakina mashiko kwenye jamii.

Nay wa mitego amponda Zitto Kabwe

Mfalme wa kudiss Tanzania, Nay wa Mitego amerejea tena kuchafua hali ya hewa kwa kutengeneza mijadala kwenye radio na kwenye mtandao kwa ngoma yake mpya, Salam Zao.


Kwenye Salam Zao, Nay ameendeela kufanya kile akifanyacho kwa uzuri (do what he does best) kuponda.


Awamu hii list ya aliowadiss imeongezeka zaidi na kuingia pia kwenye siasa huku akiendelea kuwapa madongo wana hip hop wenzie.


Ameanza kwa kumdiss Madee kwa kusema kuwa yeye ndio rais wa Manzese na kwamba Madee amesanda. “Mi ndo rais wa Manzese yule tozi kasanda, Manzese mikono juu naiongoza kamanda,” anachana Nay.


Nay wa Mitego ameendelea kuwadiss wana hip hip huku akiijita kuwa yeye ndio gangster rapper na anatengeneza hela huku wengine wakinuka vikwapa. Hakusita pia kuwarushia bombshell Weusi. “Yo Mchomvu wape salam ‘Kubumkubum’ waimbie watakufa njaa muziki umebadilika,” anarap Nay.



Nay pia amemdiss Zitto Kabwe kwa kurap:

 “Word up Diamond, mwanangu wewe si mtoto wa Kigoma, mpe salama Zitto Kabwe mwambie afanye siasa aachane na Bongo Flava huku hatumtaki kabisa, maneno mengi, propaganda hajui kutekeleza, Kigoma Allstars tayari kawatelekeza.”

Rapper huyo pia amerap kuwa wapo watu waliojipatia utajiri kutokana na misiba ya Mangwea na Kanumba.

“Wanamiliki gari, wameota na vitambi kwa hela za rambirambi, mkizingua nawataja,”anasisitiza. Anasema tangu kifo cha Kanumba Bongo Movies imekufa na haiuzi tena.


Pia hajamuacha mwanzilishi wa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen kwa kudai kuwa licha ya kuwapa zawadi kubwa washindi, wameendelea kupigika mtaani.

“Hizi Salam ziende kwa madam Rita na Bongo Star Search. Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi?! Namuona Walter Chilambo kapigika kama zamani, Haji Ramadhani kachoka yupo kitaani. Nauliza milioni hamsini zao anazila nani, acheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani.”