Friday, September 21, 2012

TBL YAKABIDHI MABASI KWA SIMBA NA YANGA

Kampuni ya Bia Tz TBL imekabidhi mabasi mawili kwa Timu hasimu za Mpira wa miguu Simba na Yanga kama sehemu ya udhamini kwa ajili ya kurahisisha usafiri kwa Timu hizo mbili.
Makabidhianao rasmi yamefanyika leo katika ofisi za TBL Jijini Dar Es Salaam(Magari hayo kama yanavyojieleza yenyewe hata sihitaji kueleza saaana)

NEY WA MITEGO AWAFUNGUKIA WANA BONGO MOVIE, AKANA KUTOKA NA NISHA

Baada ya story kuenea mtaani kuwa mkali wa Bongo Flava Ney wa Mitego anatoka kimapenzi na Mcheza Filamu ambae pia amejikita kwenye anga za muziki  Salma Jabu a.k.a Nisha, Mkali huyo wa Bongo Flava amefunguka ndani ya Hotmix jana kuwa story hizo hazina ukweli wowote ila Nisha ni mshikaji wake wa kawaida tu. Alipoulizwa kuhusu kuchagua mchumba kati ya waigizaji wa kike Bongo, Ney amefunguka kuwa kumwambia achague mchumba ndani ya Tasnia hiyo ni sawa na kumkosea heshima maana hamna Msichana anayeweza kuwa mchumba wake kutokana na tabia za wasichana wengi waliopo kwenye Tasnia hiyo. Hata hivyo Ney amezungumzia mashairi yaliyomo kwenye ngoma yake ya Nasema nao ambayo imeleta mtafaruku mkubwa baina yake na Wana Bongo Movie kuwa kila alichokizungumza kwenye ngoma hiyo yana uhakika na mfano mzuri ni mambo machafu yaliyotokea kwa baadhi ya wasichana wa Tasnia hiyo kuonekena kwenye vyombo mbalimbali vya habari wakiwa na mavazi yaliyoacha kiasi kikubwa cha miili yao kikiwa uchi. Aidha alimalizia kwa kumfananisha mwenyekiti wa Bongo Movie club Jacob Steven(JB) na wasichana kama Aunt Ezekiel na Wema Sepetu kwa kile alichodai kuwa alimtolea maneno machafu kwa kushirikiana na wasichana hao.